Naibu Waziri wa Nishati, Wakili Stephen Byabato akizungumza wakati wa Uzinduzi wa Muongozo wa Uwekezaji kwa Mkoa wa Singida, Februari 23, 2021.

Naibu Waziri wa Nishati, Wakili Stephen Byabato (Tatu kulia) akipiga makofi baada ya kuzindulia kwa Kitabu cha Muongozo wa Uwekezaji Mkoani wa Singida, Februari 23, 2021.

Naibu Waziri wa Nishati, Wakili Stephen Byabato(kushoto) na Mkuu wa Mkoa wa Singida, Rehema Nchimbi (pili kushoto) wakibadilishana mawazo na uongozi wa Mkoa huo, baada ya kuwasili katika uzinduzi wa muongozo wa uwekezaji kwa mkoa wa Singida, Februari 23,2021.

Waziri wa Nishati, Wakili Stephen Byabato (kushoto) na Mgeni Rasmi katika Uzinduzi wa Muongozo wa Uwekezaji Mkoani Singida, akimwakilisha Waziri Mkuu wa Tanzania, Kasim Majaliwa, Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais Uwekezaji, Profesa. Kitila Mkumbo wakizungumza kabla ya Uzinduzi wa Muongozo wa Uwekezaji mkoani wa Singida, Februari 23, 2021.

Naibu Waziri wa Nishati, Wakili Stephen Byabato (kulia) akitazama chupa ya Mvinyo katika mabanda ya maonyesho wakati wa Uzinduzi wa Muongozo wa Uwekezaji kwa Mkoa wa Singida, Februari 23, 2021

 

……………………………………………………………………..

Na Zuena Msuya Singida,

Naibu Waziri wa Nishati, Wakili Stephen Byabato, amewataka wawekezaji Duniani kote kuja kuwekeza mkoani Singida kwakuwa kuna Umeme mwingi wakutosha na wa uhakika.

Alisema hayo alipokuwa akizungumza wakati wa Uzinduzi wa Mwongozo wa Uwekezaji mkoani Singida, uliofanyika Februari 22, 2021.

Wakili Byabato alisema kuwa, kwa sasa mkoa huo unazalisha umeme wa Megawati 132, lakini mahitaji halisi ni Megawati 10.7 tu, hivyo kuna ziada ya Megawati 122.

Hata hivyo alisema kuwa mkoa huo pia, hivi karibuni unatarajia kukamilisha ufungaji wa mashine umba mpya itakayozalisha umeme wa Megawati 100, na hivyo kuufanya mkoa huo kuzalisha jumla ya Megawati 232, huku matumizi yakiendelea kuwa Megawati 10.7, na ziada itakuwa megawati 222.

“Wawekezaji wa ndani na nje ya nchi  hii, wenye Viwanda, Migodi, Wafanyabiasha mbalimbali na shughuli zote zinazohitaji umeme njooni Singida , tumieni hii fursa ya uwepo wa umeme mwingi, wakutosha na uhakika kuwekeza kwaku umeme ndiyo muhimili mkuu wa kuendesha shughuli zote za uwekezaji kwa kila Taifa Duniani”, alisema Wakili Byabato.

Akizungumzia usambazaji wa Umeme vijijini, Wakili Byabato alisema kuwa, Vijiji 174 vimesalia kupata umeme kati ya vijiji 298 vya mkoa mzima wa Singida, ambapo aliahidi kuwa vijiji hivyo vyote vitawekewa umeme katika Mradi wa Usambazaji wa Umeme Vijiji (REA III) mzunguko wa pili unaoendelea kutekelezwa kuanzia Mwezi Februari mwaka huu.

Kwa upande wake Mgeni Rasmi katika uzinduzi huo akimwakilisha, Waziri Mkuu wa Tanzania, Kasim Majaliwa, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Uwekezaji, Profesa. Kitila Mkumbo alisema kuwa wataalamu waliopewa dhamana ya kusimamia masuala ya uwekezaji wawe makini wakati wa mchakato wa majadiliano ya uwekezaji.

Aidha alisema kuwa ni muhimu wataalamu hao kuzielewa, kuzingatia na kuzijali na kuheshimu sheria za uwekezaji nchini kwa maslahi mapana ya nchi na wa Tanzania kwa jumla.

Prof. Mkumbo aliwasisitiza wataalamu hao kuzingatia uzalendo wa nchi na kuhakikisha kuwa uwekezaji husika unaleta tija na manufaa kwa taifa katika kuongeza uchumi badala ya uwekezaji huo kumnufaisha muwekezaji pekee. 

Sambamba na hilo wataalam hao wametakiwa kuwapenda, kuwathamini na kuheshimiana na wawekezaji katika kila sekta ili kuendelea kuwavutia wawekezaji.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...