Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo akizungumza katika kikao kazi kilichoandaliwa na Katibu Tawala wa Mkoa huo ambacho kimewajumuisha   walimu wakuu wa shule za sekondari za serikali kutoka Wilaya zote  kwa lengo la kuweza kujadili na kupanga namna ya kuweza kuboresha sekya ya elimu na kukuza kiwango cha ufaulu.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani Dk. Delphine Magere akizungumza na walimu wakuu wapatao 85 hawapo pichani kutoka shule mbali mbali za sekondari ambazo zinamilikiwa na serikali ili kujadili namna bora ya kukuza kiwango cha ufaulu kwa  wanafunzi na kujadili mikakati ya kuboresha elimu kwa ujumla.

………………………………………………………………………………

NA VICTOR MASANGU, PWANI  

MKUU wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo amechukizwa na baadhi ya walimu ambao ni wazembe katika kutekeleza majukumu yao ipasavyo katika kuwafundisha wanafunzi na kuwagiza wakuu wote wa shule za sekondari kubadilika na kuhakikisha wanaweka mipango madhubuti  ambayo itaweza kuongeza kasi ya ufundishaji ili  kuboresha  sekta ya elimu  na kusaidia kasi ya  kiwango cha ufaulu iweze kuongezeka hasa katika shule za serikali.

Ndikilo ametoa kauli hiyo wakati wa kufungua kikao kazi ambacho kimewakutanisha wakuu wa shule za sekondari za serikali wapatao 85 kutoka Wilaza zote za Mkoa wa Pwani kwa lengo la  kujadili mikakati madhubuti ambayo itasaidia kuinua   kiwango cha elimu  kwa wanafunzi na kuwataka wakuu wote wa shule kulivalia njuga suala hilo na kuwachukulia hatua kali walimu amabo ni wazembe.

Aliongeza kwamba lengo la serikali ya Mkoa wa Pwani ni kuhakikisha kwamba inaweka mipango madhubuti kwa ajili ya kuongeza kasi zaidi kwa wanafunzi wetu wa wanaosoma katika shule mbali mbali za serikali hivyo walimu wote mnapaswa kuongeza juhudi zaidi katika kutilia mkazo suala zima la kuwafundisha wanafunzi ili waweze kufanya vizuri katika  masomo yao.

“Mimi kama Mkuu wa Mkoa wa Pwani uwa nashangaa sana kuona katika shule zingine zinafanya vizuri na zingine zinafanya vibaya kwa hivyo rai yangu na maagizo kwa wakuu wote wa shule za sekondari amabzo ni zaserikali lazima sasa mhakikishe mnawafuatilia kwa ukaribu walimu wote ambao ni wazembe katika ufundishaji maana haiwezekani mwalimu anapokea mshahara lakini katika kuwafundisha wanafunzi hafanyi hivyo hii sio sahihi hata kidogo,”alisema Ndikilo.

Aidha Ndaikilo aliongeza kuwa  ili wanafunzi wa shule za serikali waweze kufanya vizuri katika mitihani yao mbali mbali ya Taifa inatakiwa kuwe  na ushirikiano wa karibu baina na walimu wakuu pamoja na walimu wa kawaida katika suala zima la kuweza kuwaandaa mapema wanafunzi ili wanapoingia katika mitihani yao wanakuwa wameshajiweka katika maandalizi mazuri.

Katika hatua nyingine Ndikilo aliwapongeza wallimu wakuu hao wa shule za sekondari za serikali kwa kuweza kujitahidi kwa ahali na mali kuongeza kiwango cha ufaulu mwaka hadi mwaka na kuwataka waendelee na moyo huo huo wa kuongeza juhudi na mahalifa zaidi ili Mkoa wa Pwani uweze kuingia katika tano bora katika ngazi ya Taifa.

 

Kwa upande wale Afisa elimu wa Mkoa wa Pwani  Khadija Mcheka  amesema kwamba licha ya kiwango cha elimu elimu ya sekondari kuongezeka  kwa asilimia 85.8  ukilinganisha na miaka iliyopita lakini bado kuna changamoto zilizopo katika sekta hiyo ikiwemo ya  miundombinu ya majengo ya madarasa, pamoja na  uhaba wa vitendea kazi ambavyo vinahitajika ili kuboresha sekta ya elimu.

Naye Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani Dk. Delphine Magere amabye ndie aliyeitisha kikao kazi hicho alibainisha kwamba dhumuni kubwa ni kuwakutanisha wakuu wote wa shule hizo za sekondari serikali ni kwa lengo la kuweza kujadili changamoto zilizopo katika sekta ya elimu ili kuzitafutia ufumbuzi na kuweka mbinu zitakazosaidia  kuongeza kiwango cha elimu.

Pia Dk. Magere aliongeza kuwa ana imani kikao kazi hicho katia ya walimu wakuu kitaweza kuleta chachu zaidi ya kukuza kasi ya maendeleo katika sekta ya elimu na kwamba katika siku zijazo wanatarajia wanafunzi wanaosoma katika shule mbali mbali za serikali wataweza kufanya vizuri zaidi tofauti na miaka iliyopita.

“Hiki kikao nimekiandaa kwa lengo la kukutana na walimu wakuu wa shule mmbali mbali za serikjali na hapa wamekuja walimu wapatao 85 kwa hivyo ni imani yangu tutaweza kufikia malengo ambayo tumejiwekea ya Mkoa wetu wa Pwani kuingia katika nafasi ya tano bora kitaifa na ili siis tunaliweza endapo tukishikamana kwa kwa sasa utaona ufaulun wetu kwa shule za sekondari umeongezea hadi kufikia alimia 85 na tutaendelea na kasi hii.”alisema Dk. Magere.

SERIKALI Mkoani Pwani kupitia kwa Katibu Tawala wake Dk. Delphine Magere imeamua kuwakutanisha kwa pamoja walimu wakuu whao 85 kutoka shule mbali mbali za serikali za Mkoa kwa lengo la kuweza kuweza kujadili changamoto mbali ,bali ili kuweza kuzitafutia ufumbuzi lengo ikiwa ni kuongeza kasi zaidi ya ufaulu kwa wanafunzi.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...