Na  Linda Shebby  Pwani
WAZIRI wa Wizara ya Mambo ya Ndani George Simbachawene ametoa wito kwa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa NIDA kuhakikisha wanatoa vitambulisho  vipatavyo Milioni 12  ambavyo  wahusika tayari wamepewa namba ifikapo Julai mwaka  huu 2021.

Akizungumza  na waandishi  wa habari  alisemamkuwa  katika ziara hiyo  ilikua nanmalengo ya kwenda  kuangalia  uwezo wa Nida pamoja na mitambo yao mipya ambapo pia aliweza kukagua maeneo mbalimbali   ya jengo hilo na baada ya hapo amesema ameridhika na hali  ya mazingira na uwezo wa miitambo hiyo   mipya   yenye uwezo   uwezo  wa kuzalisha vitambulisho  1000 hadi 1200  kwa saa pia  mitambo hiyo ina uwezo  wa kuzalisha kadi 72,000 kwa saa 16.

"Nimewaambia  NIDA kwa kushirikiana na  Taasisi zote  waweke huduma kwenye   vitambulisho  hivyo vya taifa ili  viweze kutumika kwa huduma zingine muhimu  ikiwa ni pamoja na Bima ya Afya na Kibenki   , tumeliona  hilo  na  kwamba  halina  tatizo la kiufundi na linaweza kufanyika  bila  kuathiri jambo  lolote" alisema Simba Chawene.

Aidha alitoa maelekezo kwa Nida  kuwa wanatakiwa  watoe vitambulisho hivyo katika kila mkoa  nchini  kwa sababu kila mwananchi ambaye alipata namba anahitaji  kuwa na kitambulisho.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene (kulia), akiangalia kitambulisho kilichokamilika baada ya kuhakikiwa katika Kitengo cha kuhakiki ubora wa kadi zilizozalishwa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Mjini Kibaha, Mkoani Pwani, leo.   Simbachawene alitembelea Kituo cha Kanzidata cha NIDA na amesema kuwa, wananchi wote waliotambuliwa na kupewa namba ambao ni zaidi ya Milioni 12, ifikapo mwezi Julai Mwaka huu watakuwa wamepata vitambulisho vyao. Wapili kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa NIDA, Dk. Anorld Kihaule.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene, akizungumza na Waandishi wa habari (hawapo pichani) baada ya kutembelea Kituo cha Kanzidata cha Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Kibaha, Mkoani Pwani, leo. Amesema wananchi wote waliotambuliwa na NIDA, na kupewa namba ambao ni zaidi ya Milioni 12, ifikapo mwezi Julai Mwaka huu watakuwa wamepata vitambulisho vyao. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa NIDA, Dk. Anorld Kihaule.

 

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene (kushoto), akimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo, kabla ya kuanza ziara yake Mjini Kibaha leo, kutembelea Ofisi za Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA). Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa NIDA, Dk. Anorld Kihaule, na wapili kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Mhandisi, Martin Ntemo.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene (kushoto), akisalimiana na Maafisa wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Mjini Kibaha, Mkoani Pwani, leo, wakati alipokuwa anawasili mjini humo kwa ajili ya kutembelea ofisi za NIDA Mkoani humo. Amesema wananchi wote waliotambuliwa na NIDA, na kupewa namba ambao ni zaidi ya Milioni 12, ifikapo mwezi Julai Mwaka huu watakuwa wamepata vitambulisho vyao. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...