Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV

MASHABIKI wa Soka la Tanzania wamejionea wenyewe na sasa wameamini katika Uwanja wa Benjamin Mkapa hajawahi kutoka mtu, maana yake hakuna timu iliyoifunga Simba SC katika Uwanja huo wa nyumbani katika nyakati hizi za Uwakezaji wa Mfanyabiashara Mohammed Dewji ‘MO’ ikiwa katika mchakato wa mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji wa klabu hiyo (Mfumo wa Hisa).

Kwa nyakati hizi usajili wa Kikosi uliofanywa na Uongozi wa Klabu hiyo si wakawaida, Simba SC kwa sasa ina Kikosi imara cha mashindano ambacho kimaweza kushindana na timu yoyote barani Afrika na hata duniani.

Imedhihirika katika mchezo wa raundi ya Pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly SC ya Misri mchezo uliopigwa kwenye dimba hilo lililopewa jina la Estadio de Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam. Simba SC walimaliza mchezo kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya timu hiyo ngumu na bora barani Afrika na kukusanya alama Sita huku wakiongoza Kundi ‘A’ la Michuano hiyo.

Inaafahamika, Al Ahly SC ni timu bora Afrika na hata duniani kwa ujumla na ubora wao unaotokana na kukusanya mataji mengi katika historia yao ya soka hasa soka la Afrika, tuendelee kuamini Al Ahly ni bora zaidi  barani Afrika, ndio! ni bora wana historia ya mataji tisa ya CAF CL kabatini kwao, na pia ni Mabingwa Watetezi wa Michuano hiyo msimu huu.

Hivi karibuni wametoka kushiriki Mashindano ya Kombe la Vilabu la Dunia nchini Qatar ambapo Bayern Munich walitwaa Ubingwa wa Michuano hiyo msimu huu huku Mabingwa wa Afrika wakimaliza nafasi ya tatu baada ya ushindi wa mikwaju ya Penalti 3-2 dhidi ya Sociedade Esportiva Palmeiras ya Brazil, walifunga timu ya Al-Duhail ya Qatar bao 1-0 na walifungwa na Bayern bao 2-0.

Mabingwa Watetezi wa Tanzania, Simba SC msimu huu wakiwa bora tayari wameshinda michezo miwili ya mwanzo dhidi ya AS Vita (1-0) ugenini mjini Kinshasa, DR Congo na ushindi wa nyumbani dhidi ya miamba Al Ahly SC (1-0) katika Kundi A.

Simba SC mara ya mwisho kutupwa nje ya Michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika ilikuwa msimu wa 2019-2020 dhidi ya UD Songo ya Msumbiji baada ya sare ya 0-0 ugenini na sare ya 1-1 nyumbani (Uwanja wa Benjamin Mkapa).

Msimu wa 2018-2019 wakiwa na Kocha Mkuu, Patrick Aussems walifuzu makundi ya Michuano hiyo kwa kuifunga Nkana FC ya Zambia mchezo wa mwisho kwa jumla ya mabao 4-3 baada ya kufungwa 2-1 mjini Kitwe, Zambia na ushindi wa bao 3-1 Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Hatua ya Makundi msimu huo, Simba SC walifanikiwa kushinda mechi zote za nyumbani, dhidi ya JS Soura 3-0, Al Ahly 1-0 na AS Vita Club 2-1 lakini Simba SC walifungwa michezo yote mitatu ya ugenini, dhidi ya JS Soura (Algeria) walifungwa bao 2-0 na Al Ahly (Misri) bao 5-0 na AS Vita (DR Congo) bao 5-0.

Tazama sasa msimu huu wa 2020-2021 waliwatupa nje ya Michuano, Plateau United ya Nigeria kwa jumla ya bao 1-0 bao pekee lililofungwa ugenini nchini Nigeria katika mji wa Jos bao pekee la Clatous Chota Chama, mchezo wa marudiano Simba SC walitoka sare ya 0-0 katika uwanja wa nyumbani, Benjamin Mkapa na kufuzu raundi inayofuata.

Katika raundi hiyo ya mtoano (Play Off) Simba SC walikutana na FC Platinum ya Zimbabwe ambapo waliruhusu bao 1-0 ugenini katika dimba la National Sports mjini Harare, Platinum walipokuja nchini Tanzania kwa mchezo wa marudiano walipokea kichapo cha bao 4-0 kutoka kwa Mnyama na Simba SC kufuzu hatua ya makundi ya Michuano hiyo ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Hata hivyo, Wekundu wa Msimbazi, Simba wana historia nzuri ya kuzifunga timu za Waarabu katika Mashindano hayo ya Ligi ya Mabingwa Afrika na hata Kombe la Shirikisho Afrika katika nyakati tofauti.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...