Na Said Mwishehe, Michuzi TV


SERIKALI ya Ufaransa kupitia Rais wake Emmanuel Macron imesema katika kukabiliana na homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi vya Corona asilimia tano ya chanjo zake itazisambaza katika nchi mbalimbali barani Afrika.

Hivyo Rais Macron amezitaka nchi nyingine tajiri zikiwemo za Ulaya na Marekani nazo kufanya hivyo kama hatua ya kushirikiana katika kukabiliana na janga la Corona.

Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Frederic Clavier amesema nchi zenye uchumi mkubwa ni lazima waoneshe ushirikiano kwa nchi za uchumi wa chini na kati kwa kuwahakikishia upatikanaji na usambazaji wa haraka wa chanjo hizo na Serikali ya Ufaransa kupitia Rais wao Macron imeshaamua asilimia tano ya chanjo zake itakwenda barani Afrika.

"Ili kukabiliana na janga hili la Corona ambalo limeendelea kutesa nchi nyingi duniani, ni vema tukawa na mbinu mbalimbali za kukabiliana na janga hili, Rais wetu Macron ameelezea hatua ambazo nchi yetu inachukua katika kusaidia bara la Afrika kupata chanjo hizo,"amesema Balozi Clavier na kuongeza kwamba " nitashirikiana na kufanya kazi kwa karibu na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Wazee katika mwito uliotolewa na Rais Macron".

Kupitia taarifa hiyo ameeleza katika mkutano wa G7 wa Baraza la Ulaya, Rais Macron alitoa ushauri kwa mataifa yenye uchumi mkubwa na tajiri kama nchi ya Marekani, nchi za Ulaya kutenga asilimia tatu hadi tano ya chanjo zake ili kuzisaidia nchi za Afrika huku akifafanua utaratibu huo uhusishe kwa nchi hizo kuchangia chanjo kwa kuziuza kwa gharama nafuu kama msaada kwa nchi zenye kipato cha chini.

Aidha mahojiano kati ya Rais Macron na gazeti la Financial Times yaliyofanyika Februari 17,2021 alizungumzia umuhimu wa kuhakikisha usambazaji wa chanjo hizo unafanyika kwa haraka.
Rais Macron alisisitiza wao si kisiwa, watu wao zaidi ya Milionil 10 wana familia katika maeneo mbalimbali duniani na kwamba katika dunia hii yenye kila aina ya utandawazi chanjo isiwe ya ubaguzi."Ni vema chanjo ikatolewa kwa watu wote kadri itakavyowezekana."

Katika kuhakikisha jitihada hizo ziafanikiwa hasa wa kuharakisha usambazaji wa chanjo, wadau wa kimataifa wameunganisha nguvu zao na kuchangia Mabilioni ya Dola za Marekani kwa COVAX ambayo ni programu maalum ya Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) katika kupambana na corona.
 Pamoja na hayo taarifa hiyo imefafanua kwenye kikao cha G7 kilichofanyika kwa njia ya mtandao Februari 19, 2021 ikiwa ni mara ya kwanza tangu Aprili mwaka 2020, mchango uliongezeka hadi kufikia Sh.Bilioni 7.5.

Wakati huo huo Rais Macron alizishauri jumuiya za kimatiafa kuzisaidia nchi za Afrika kupata chanjo kuliko kuwafikiria watu wake peke yake."Wafanyakazi wa afya katika Mji wa Dakar nchini Somalia wanahitaji chanjo kwa haraka.Hivyo Ufaransa tumekuja na jitihada za G7 katika kuitaka  Ulaya na Marekani kusambaza dozi milioni 13 hasa kwa wafanyakazi wa afya milioni 6.5 walioko Afrika". 

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron

Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Frederic Clavier

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...