Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo  na Mbunge wa jimbo la Mkuranga,Abdallah Ulega ametoa mifuko 340 ya saruji pamoja na Fedha taslimu zaidi ya milioni nne na Mabati 30 za kuanzishia ujenzi wa shule za Msingi na Sekondari  pamoja na Zahanati katika kata za Vianzi,Mipeko,Nyamato na Kimanzichana

Shule  hizo alizozichangia ni shule ya msingi Kisima inayojengwa kata ya Vianzi shule ya msingi Kisiwani inayoanzishwa katika kata ya Mipeko  Shule ya  Sekondari ya kata ya Kimazichana Shule ya msingi kijiji cha Mkiu kata ya Nyamato, Zahanati ya kimanzichana Magharibi na Zahanati ya kimazichana Kaskazini Wilayani Mkuranga mkoani Pwani.

Akizungumza na wanachi wakata hizo kwa nyakati tofauti  wakati wa ziara yake ya kutoa shukrani kwa wananchi pamoja na kukagua miradi ya maendeleo aliyoifanya hapo jana katika kata hizo nne,Ulega amesema hatua ya  ujenzi huo umekuja kutokana na changamoto ya mrundikano wa wanafunzi madarasani pamoja na umbali mrefu wanaotembea wanafunzi kufuata elimu.

"Wanafunzi wanatembea umbali wa zaidi ya kilomita 5 kufuata shule,wanavuka mito,kiukweli wanakutana na changamoto nyingi zinazohatarisha maisha yao hali inayowapa hofu wazazi,hivyo kukamilika kwa shule hizo kutapunguza changamoto kwa kiasi kikubwa katika maeneo husika". Amesema Ulega.

Aidha Ulega pamoja na kutoa  mifuko ya saruji  na pesa taslimu pia  ameshiriki  kuchimba  msingi wa ujenzi wa  shule ya msingi Kisiwani kata ya Mipeko kwa kushirikiana na wananchi pamoja na diwani wakata  hiyo,Adili Kinyenga ili kuendelea kuhamasisha maendeleo Mkuranga.

Hata hivyo ametoa wito kwa wananchi kuendelea kujitolea kwa hali na Mali na kuwaahidi kuendelea kuwaunga mkono ilikufanikisha ujenzi wa shule hizo,ili kutatua changamoto za kielimu Mkuranga.

Kwa upande wa madiwani wa kata hizo  wakiwakilishwa na diwani wa kata ya Mipeko,Adili kinyenga  amemshukuru Mbunge wa jimbo  kwa juhudi zake za kusaidia wananchi na kuahidi kuisimamia shule  pamoja na zahanati  zinakamilika kwa wakati.

Sanjari na hayo Ulega ametembelea daraja la Mipeko na kumtaka diwani,kwa kushirikiana na wananchi kuona namna ya kupatikana kwa kivuko cha muda kabla ya mvua za masika kuanza kitakachowezesha wananchi kuvuka  wakati serikali ikipambana kupatikana kwa daraja la kudumu katika eneo hilo.

Hata hivyo hapo awali serikali ilishatumia kiasi cha shilingi milioni 200 kujenga daraja katika eneo hilo kabla mvua kubwa za mwaka Jana kuliharibu,hivyo Ulega amesema yupo tayari kushirikiana na wananchi pamoja na diwani kuhakikisha kivuko cha muda kinapatikana ilikuondoa adha kwa wananchi wa kata ya mipeko.

Mbunge wa jimbo la Mkuranga na Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo,Abdallah Ulega akishiriki kufyatuwa matofali kwaajili ya ujezi wa  shule ya msingi  Kimanzichana Kusini jana katika ziara yake ya kutoa shukrani kwa wananchi pamoja na kukagua miradi ya maendeleo.(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)Mwenyekiti wa Halmashauri Mkuranga, Mohamed Mwela wakishiriki kufyatuwa matofali kwaajili ya ujezi wa  shule ya msingi  Kimanzichana Kusini jana katika ziara yake ya Mbunge ya shukrani kwa wananchi pamoja na kukagua miradi ya maendeleo.Mbunge wa jimbo la Mkuranga na Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo,Abdallah Ulega akiwakadhi  viongozi wa Kijiji cha Mkiu kata ya Nyamato  bati 30 Saruji mifuko 60 Pamojana fedha  laki tano ya kwaajili  ya Shule ya msingi Mkiu.Mbunge wa jimbo la Mkuranga na Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo,Abdallah Ulega akiwakabidhi viongozi wa kijiji cha Kilamba fedha milioni moja kwaaji ya Sekondari ya kata Nyamato.Katibu wa CCM  wilaya ya Mkuranga,Said King'eng'ena(katikati)akisikiliza kero za wananchi wa wilaya hiyo na kuwaahidi kuzitatuwa kwa kushirikiana na Mbunge wa jimbo hilo.
Mbunge wa jimbo la Mkuranga na Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo,Abdallah Ulega akiwa ameambatana na Viongozi mbalimbali wakikaguwa daraja la  Mipeko na kumtaka diwani kwa kushirikiana na wananchi kuona namna ya kupatikana kwa kivuko kitakachowezesha wananchi kuvuka.(Picha zote  Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)
kazi ikiendelea ya kukaguwa miradi ya maendeleo


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...