Afisa Mkuu wa Fedha wa Benki ya NMB Benedicto Baragomwa (katikati,) akizungumza katika droo ya mwisho ya fainali ya kampeni ya MastaBata Sio Kikawaida iliyoendeshwa na benki hiyo ambapo washindi 12 wamepatikana katika fainali hiyo na kujizolea zawadi zenye thamani ya shilingi milioni nane kila mmoja, Kushoto ni Elibariki Sengasenga Mkaguzi  kutoka Bodi ya Michezo ya kubahatisha nchini na kulia ni Mwanahabari na balozi wa Benki ya NMB Masoud Kipanya, Leo Mkoani Dar es Salaam.
Wafanyakazi wa benki ya NMB na wanahabari wakifuatilia fainali ya Kampeni ya Mastabata Sio Kikawaida.

Mchakato wa kuwatafuta washindi wa fainali ya  kampeni ya MastaBata Sio Kikawaida ukiendelea.




Matukio mbalimbali wakati wa hafla ya kuwatafuta washindi kumi na mbili wa kampeni ya MastaBata Sio Kikawaida iliyoendeshwa na benki ya NMB.

KAMPENI ya MastaBata Sio Kikawaida iliyoendeshwa na Benki ya NMB imefikia tamati leo na jumla ya washindi 12 wamepatikana huku kila mmoja akijinyakulia zawadi yenye thamani ya shilingi milioni nane.

Akizungumza wakati wa hafla ya kuwapata washindi hao, Afisa Mkuu wa Fedha wa Benki ya NMB, Benedicto Baragomwa amesema katika fainali ya kampeni hiyo wateja hao wamepata nafasi ya kuchagua zawadi mbili ambazo ni kutembelea vivutio vya ndani vya utalii vya Serengeti, Ngorongoro na visiwa vya Zanzibar pamoja na bidhaa za nyumbani ikiwemo  TV inchi 50 iliyounganishwa na kifurushi kwa miezi mitatu, jokofu la kisasa la milango miwili, kompyuta mpakato iliyounganishwa na printa, simu janja (Samsung A70,) water dispenser pamoja na Microwave.

Benki ya NMB bado inaendealea na kampeni kabambe katika kuhakikisha wateja wao wananufaika na kwa sasa wapo na kampeni ya 'Bonge la Mpango' ambayo wateja watapata nafasi ya kushinda pesa, bajaji na gari jipya aina ya Fortune lenye thamani ya shilingi milioni 165 katika Grand finale.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...