Mkurugenzi wa maziwa ya Asas Ahmed Salim Abri akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa timu ya Lipuli na Bajaji
…………………………………………………………………..
NA DENIS MLOWE, IRINGA
MKURUGENZI
wa uzalishaji wa kampuni ya maziwa ya Asas, Ahmed Salim Abri, ameahidi
kuwalipia mashabiki 100 kutoka umoja wa madereva Bajaji mkoa wa Iringa
kuingia katika mchezo wa ligi soka daraja la kwanza Kati ya Lipuli Fc
dhidi ya Kengold unaotarajiwa kupigwa katika uwanja wa Samora hivi
karibuni.
Lengo
la kuwalipia tiketi hizo ni kuwahamasisha wananchi wa mkoa wa Iringa
kurudisha ushabiki wa soka na kuipa hamasa timu ya Lipuli kuibuka
kidedea katika mchezo huo na kufanikisha lengo la kuirudisha ligi kuu
soka Tanzania bara.Ahadi
hiyo aliitoa wakati wa mchezo wa kirafiki Kati ya Lipuli fc na Bajaji
FC ambapo Lipuli iliibuka na ushindi wa magoli 4 – 1 ukiwa na lengo la
kuu la kujenga mahusiano kati ya madereva Bajaji na timu ya Lipuli.
Akiongea
katika ufunguzi wa Mchezo huu Ahmed Salim ambaye alikuwa mgeni rasmi
alisema kuwa lengo ni kurudisha hamasa ya mchezo wa soka mkoani hapa
ambapo ulipotea mara baada ya timu kushuka daraja
Kutokana
na Hilo atahakikisha wanarejesha hamasa ya mashabiki kuingia uwanjani
ambapo kwa kuanza atawalipia madereva bajaji tiketi 1000 kwenye mchezo
wa Lipuli dhidi ya Kengold.
“Kwa
kutambua umuhimu wa mashabiki kwenye mchezo huo muhimu ambapo tunaamini
uwepo wao utakuwa chachu ya mafanikio kwenye mchezo huo na kuwapa Nguvu
wachezaji waibuke na ushindi na kuelewa kwamba Wana Iringa wako nyuma
yao”Alisema
Nao
viongozi wa Bajaji , Merab Kihwele akiwa sambamba na katibu wake ndugu
Bryson wameahidi kuendeleza uhusiano ambapo wameuanzisha na pia
wameahidi kuwa endapo Lipuli itaibuka kidedea watawanunulia mbuzi
wachezaji ili wale kama sehemu ya pongezi.
Aidha
wameahidi kuwa sehemu kubwa ya hamasa huku wakitumia vyombo vyao vya
usafiri kuhamasisha abiria wengine kufika uwanjani kuwashangilia Lipuli.
Kwa
upande wao uongozi wa Lipuli fc wmeahidi kuulinda na kuuendeleza
urafiki huu huku wakiamini kuwa hawa ni sehemu ya kundi muhimu ambalo
litatutasaidia sana kwenye mipango yetu ya kuipandisha timu.
Aidha
wamemshukuru mkurugenzi Ahmed Salim Abri kwa kuwapa hamasa madereva
bajaji na kushukuru viongozi wa bajaji na madereva wa bajaji kwa
kukubali kuwa wamoja katika lengo la kuipandisha timu.Wakati huo huo mmoja ya wakurugenzi wa kampuni ya Asas,
Feisal Abri ametoa kiasi cha shilingi 400000/= kwa ajili ya kununulia jezi za Mazoezi kwa timu yetu ya Lipuli.
Uongozi
wa Lipuli FC unapenda kumpongeza sana Feisal kwa mchango wake huo kwani
umekuja wakati muafaka ambapo timu ilikuwa inauhitaji sana na jezi za
Mazoezi.
“Uongozi
unatoa shukrani za dhati kwa ndugu Faisal kwani licha ya msaada wa leo
lakini pia amekuwa mtoaji wa mara kwa mara kwenye klabu yetu na amekuwa
mwepesi kila anapoombwa kuisaidia timu”
Aidha
klabu inapenda kuwakumbusha na wengine kuichangia timu yetu kwani
inauhitaji mkubwa sana. Kipindi hiki ni kipindi ambacho tunatakiwa
kuiandaa sana timu hivyo fedha nyingi zinahitajika kwahiyo tunatoa wito
kwa wadau mbalimbali kuiunga mkono timu ili hatimaye tuweze kupanda
Daraja kama ilivyo matarajio.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...