NA VICTOR MASANGU, BAGAMOYO

 JUMUIYA ya Tawala  za mitaa Tanzania (ALAT)   Mkoa wa Pwani hatimaye imefanya uchaguzi wake mkuu na kufanikiwa kupata safu mpya  katika nafasi mbali mbali za  viongozi wataoongoza kwa kipindi cha miaka mitano  ambapo Mwenyekiti kutoka halmashauri ya Chalinze Wilayani Bagamoyo Geofrey Kamugisha   akifanikiwa kuchaguliwa na wajumbe wa mkutano huo baada ya kupata kura 21 kati ya kura 38 zilizopigwa.

Katika uchaguzi huo ambao ulifanyika katika ukumbi wa halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo ulihudhuliwa na viongozi mbali mbali wa serikali ambapo katika nafasi ya Makamu mwenyekiti iliweza kuchukuliwa na Zuberi Kizwezwe ambaye pia yeye ni Mwenyekiti mpya kutoka halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe kwa kupigiwa kura zote 38 za ndio kutokana na nafasi hiyo kugombea peke yake,

Pia wajumbe wa uchaguzi huo waliweza kufanya maamuzi ya kumrudisha katika kiti chake cha Katibu wa ALAT Mkoa wa Pwani Mussa Gama amabye pia yeye ni  Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe kwa kuweza kuibuka kidedea baada ya kupata kura zote 38 za ndiyo na kufanikiwa kubaki katika nafasi hiyo.

Kwa upande wa wajumbe wa nafasi katika kamati ya utendaji zilikwenda kwa Samira Mussa, Mohameddi Mwera, Fatuma Latu, Ramadhani Possy, pamoja na Hawa Mchafu ambaye ni Mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Pwani  kupitia tiketi ya  chama cha mapinduzi (CCM).

Kwa upande wake Katibu Tawala wa mkoa wa Pwani Dk. Delphine Magere ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mkutano huo  amewata viongozi wapya wa Alat kuhakikisha kwamba wanasimamia vema miradi mbali mbali ya maendeleo pamoja na kuweka mikakati madhubuti ambayo itaweza kusaidia kuinua ukusanyaji wa mapato.

“Kwa kweli kitu kikubwa ambacho ninawaomba viongozi wote ambao mmechaguliwa katika uchaguzi huu wa jumuiya ya Tawala za mitaa Tanzania Alat tawi la Mkoa wa Pwani kujikita zaidi katika kuwatumikia wananchi mbali mbali kwa kuweza kuwaletea maendeleo chanya pamoja na kusimamia miradi mbali mbali ya maendeleo,”alisema Dk Magere.

Pia katiha hatua nyingine aliwawakumbusha wenyeviti wote wa halmashauri za Mkoa wa Pwani kuhakikisha wanaweka mipango madhubuti ya upatikanaji wa kuongeza ukusanyaji wa mapato kwa kuweza kubuni  vyanzo vipya vya mapato amabvyo vitaweza kusaidia kwa kisi kikubwa kukuza zaidi kasi ya uchumi.

Kadhalika amewahimiza wakurugenzi wote kuhakikisha kwamba wanaongeza juhudi katika suala zima la ukusanyaji wa kodi mbali mbali za majengo, ushuru, pamoja na mabango ambayo yakitiliwa mkazo yataweza kuongeza zaidi ukusanyaji wa mapato katika halmashauri mbali mbali zilizopo katika Mkoa wa Pwani.

Nao baadhi ya viongozi wapya ambao wamechaguliwa katika uchaguzi huo akiwemio Katibu wa Alat Mkoa wa Pwani Mussa Gama alisema kwamba amepokea maelekezo na maagizo ambayo yametolewa na Katibu Tawala na kwamba atahakikisha kwamba anashirikiana bega kwa bega na wenzake katika kufanya kazi kwa bidii na kusimamia miradi ya maendeleo kwa ajili ya kuwasaidia wananchi wa Pwani,

Naye Mwenyekiti Mpya wa Alat Mkoa wa Pwani Geofrey Kamugisha alibainisha kwamba atasimamia sheria na taratibu zote kwa mujibu wa katibu sambamba na kuzingatia maelekeo yote ambayo wameelekezwa ikiwemo suala zima la kutatua migogoro ya ardhi kati ya wakulima na wafugaji ili iweze kumalizika na wananchi washiriki kikamilifu katika shughuli za kuleta maendeleo

 Nao baadhi ya wabunge wa Mkoa wa Pwani ambao walishiriki kikamilifu katika mkutano huo akiwemo Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani, Kikwete, Mbunge wa Jimbo la Rufiji Mohamed Mchengerwa pamoja na Mbunge wa Jimbo la Bagamoyo wameahidi kutoa ushirikiano wa hali na mali kwa safu hiyo ya uongozi wa Alat Mkoa wa Pwani lengo ikiwa ni kuweka misingi imara amabyo itasaidia kutatua changamoto za wananchi.

Mkutano huo wa Uchaguzi mkuu wa Jumuiya ya Tawala za mitaa Tanzania (ALAT) Mkoa wa Pwani ulihudhuliwa na wajumbe mbali mbali ambao ni wenyeviti wote kutoka halmashauri tisa,baadhi ya madiwani, wabunge,  wakurugenzi wa halmashauri pamoja na viongozi wa serikali kutoka ngazi za Wilaya pamoja na Mkoa.


Katibu wa Jumuiya ya Tawala za mitaa Tanzania (ALAT) Mkoa wa Pwani Mussa Gama ambaye pia ni mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe akitoa neno la shukrani kwa wajumbe wa mkutano huo maalumu wa uchaguzi baada ya kuchaguliwa kwa kupata kura zote 38 za ndio ili aweze kubaki katika kiti chake cha ukatibu.

Mwenyekiti mpya wa ALAT Mkoa wa Pwani kushoto Geofrey Kamugisha akiwa wameketi meza kuu pamoja na Makamu wake mara baada ya kumalizika kwa uchaguzi huo ambao ulifanyika katika ukumbi wa halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo.

Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete akiwa sambamba na baadhi ya wajumbe wengine katika mkutano huo wakiwa katika sanduku kwa ajili ya kuweza kupiga kura na kumchagua kiongozi ambaye ataweza kuwaletea mabadiko ya kimaendeleo katika Nyanja mbali mbali.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani Dk. Delphine Magere ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mkutano huo wa uchaguzi wa Alat Mkoa akiwa anazungumza na wajumbe hawapo picha ambao waliohudhulia katika mkutano huo maalumu kwa ajili ya  zoezi la upigaji wa kura za kutafuta viongozi.

Katibu wa ALAT Mkoa wa Pwani Mussa Gama akitoa ufafanuzi kwa baadhi ya wagombea ambao walishiruki katika  kugombea nafasi ya uenyekiti wa Jumuiya hiyo uliofanyika Wilayani Bagamoyo. Caption- 6 Pic

Picha ya Mwonekano  wa wajumbe kutoka katika halmashauri mbali mbali za Mkoa wa Pwani ambao waliweza kushiriki katika uchaguzi huo ambao uliwakutanisha jumla ya wajumbe 38 ambao waliweza kupiga kura na kuchagua viongozi.


Wajumbe wa mkutano huo wa uchagzui wa Alat Mkoa wa Pwani wakiwa katika zoezi la upigaji wa kura katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo.([PICHA NA VICTOR MASANGU)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. It really helpful blog article for us, I have also found interesting blog website related to technology, email migration, and data recovery. You can comfortably convert your outlook OST file data into PST file formats just with the help of Cheapest OST to PST Converter Software with highlights features.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...