Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV

Afisa Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Simba, Barbara Gonzalez amesema kuwa sababu za kiufundi ndio zimefanya Mchezaji Bernard Morrison kuachwa kwenye kikosi cha timu hiyo iliyoenda Sudan kwa mchezo wake wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya wenyeji El Merreikh.

Katika mazungumzo yake na Waandishi wa Habari kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam baada ya kutua nchini Tanzania, Barbara amesema Morrison ni Mchezaji mzuri, mwenye nidhamu katika Kikosi cha Simba SC

Kuhusu taarifa za Mchezaji huyo kugomabana na Kocha Didier Gomes Da Rosa, CEO Barbara amesema ni uzushi taarifa hizo si za kweli, ameshauri Waandishi wa Habari kutoa taarifa zenye ukweli na uhakika kwa kuzifanyia upembuzi yakinifu kabla ya kuzitoa kwa jamii.

“Hili taarifa zinazoenea mitandaoni si za kweli ni uzushi na uongo, Waandishi wa Habari lazima watumie Uandishi wa Habari wa Kiuchunguzi (Investigative Journalim) ili kupata uhakika wa stori ambayo unataka kuitoa kwa jamii”, amesema Barbara.

Pia Barbara amesema taarifa hizo zinamkumbusha taarifa za nyuma kati ya Mshambuliaji wa timu hiyo, Medie Kagere na Aliyekuwa Kocha Mkuu wa Kikosi hicho, Sven Vandenbroeck.

“Mimi naona haisaidii, naona haijengi Mpira wetu, leo tungekuwa tunazumgumzia Simba SC imerejea baada ya kutoa sare na El Merreikh nyumbani kwao Sudan, labda Simba SC sasa infanye nini katika michezo yake ijayo”, ameeleza Barbara.

Hivi karibuni katika mitandao ya kijamii, kulienea tetesi za Mchezaji huyo wa Simba SC, Bernard Morrison kuachwa na Kocha Mkuu wa timu hiyo kutokana na kutoelewana na baina yao.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...