Timu za watani wa jadi katika soka la Wanawake kati ya Simba Queens dhidi ya Yanga Princess, imechezwa jioni ya leo Ijumaa 05/03/2021 katika dimba la Uhuru Wilaya ya Temeke, Dar es salaam.

Katika mchezo huo Simba Queens imefanikiwa kuibuka na ushindi mnono wa magoli 3 kwa 0 dhidi ya mahasimu wao Yanga Princess.

Magoli ya Simba yamefungwa na Nahodha Mwanahamisi Omary (30), Opah Clement  (Penati, 43) na Joel Bukuru (50).

Kwa matokea haya ya leo, Simba Queens inashika usukani wa ligi ya wanawake kwa kuwa na Point 39 huku wakiwaacha watani wao nyuma kwa pointi moja yaani wakiwa na pointi 38.

Mtanange huo umeenda sambamba kabisa matukio yanayohusisha shughuli za Wanawake kuelekea kilele cha Siku ya Wanawake Duniani kinaadhimishwa machi 08, 2021. ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni Mwanamke #ChaguaKupambana.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...