Charles James, Michuzi TV
SIKUOTA! Hii ni kauli ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango baada ya kuapishwa na Rais Samia Suluhu Hassan kushika nafasi hiyo leo Ikulu, Chamwino Dodoma.

Dkt. Mpango amesema nafasi aliyoteuliwa hakuwahi kuiota kuishika ambapo amemuahidi Rais Samia kuwa hatomsaliti kama ambavyo Yesu alisalitiwa na mwanafunzi wake Yuda Eskarioti kwa vipande 30 vya fedha.

"Mimi mtoto wa maskini sikuota kushika nafasi hii, nakuahidi nitatekeleza kwa bidii kazi zote utakazonielekeza na kazi zingine za katiba kama ilivyoelekezwa kwenye ibara ya 40, niko tayari kufanya kazi, nitume usiku na mchana hasa kufanikisha Ilani ya CCM.

Na katika kutekeleza majukumu hayo yote ntashirikiana na viongozi wote wa pande zote mbili za muungano, mihimili yote mingine na zaidi viongozi wengine." Amesema Dkt Mpango.

Makamu wa Rais Dkt Mpango ambaye alikua ni Mbunge wa Jimbo la Buhigwe ametoa rai kwa wananchi wa Jimbo hilo kuhakikisha wanamchagua Mbunge anayetokana na Chama cha Mapinduzi CCM ambaye ataletwa na chama hicho.

"Nishukuru pia kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama kwa kulipitisha jina langu, niwashukuru wananchi wangu wa Buhigwe kwa kunipa imani yao kwangu kwa kunichagua, naamini hiko kibali pia kimetoka kwa Mungu na kimesaidia wewe Rais kuniteua." Amesema Dk Mpango

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...