Wanawake wajasiriamali 50 wanufaika na Halotel siku ya wanawake duniani.



. Katika kuazimisha siku ya wanawake duniani, kampuni ya Halotel Tanzania imesherekea kwa kuunga mkono juhudi za wanawake katika majukumu yao ya kujikomboa kiuchumi na kujenga taifa kiujumla.

Kutokana na ukweli kwamba wanawake wamekuwa wadau na mstari wa mbele katika kujikwamua kiuchumi, kifikra na kusaidia jamii, Kampuni ya simu ya Halotel imethamini jitihada hizo kwa kutoa msaada wa hali na mali kwa wanawake hawa ikiwa ni katika kutambua juhudi zao kubwa kwa namna mbalimbali.

Halotel imetoa mifuko hamsini (50) ya chakula na malazi kwa wakina mama 50 katika soko la Mwananyamala jijini Dar es salaam, ikiwa ni zawadi kwa wakina mama hawa wanaopambana kila siku kujitafutia riziki. Zawadi hizo ziliwasilishwa na wafanyakazi wanawake wa kampuni ya Halotel kama moja wapo ya namna ya ya kusherekea siku ya wanawake duniani.

Akitoa ufafanuzi katika zoezi la kukabidhi zawadi hizo kwa wanawake katika Soko la Mapinduzi lililoko Mwananyamala Mkuu wa Idara ya Masoko Halotel Sakina Makabu alisema "wanawake wengi wamekuwa wakifanya kazi kwa bidii ili kuboresha hali zao za kiuchumi na kusaidia jamii, kama Halotel, tunathamini na kutambua juhudi zao kwa kile wanachofanya na kutoa msaada kwao.”

‘Tunafurahi kusherekea na wanawake wenzetu kwa kutoa zawadi za mahitaji ya nyumbani lakini pia kupata wasaha wa kubadilishana mawazo’ aliongeza Sakina.

Halotel imewashukuru wanawake wote ambao wamekuwa wakipambana katika kuikwamia katika Nyanja mbalimbali za maisha na kuwapongeza katika kusheherekea siku ya kimataifa ya wanawake Duniani.




Kampuni ya simu ya Halotel imetoa zawadi kwa wanawake Hamsini (50) katika kusheherekea siku ya wanawake Duniani. Wafanyakazi wanawake kutoka idara mbalimbali Halotel walishiriki kutoa zawadi za mahitaji ya nyumbani kwa wanawake wajasiliamali katika Soko la Mapinduzi lililopo Mwananyamala jijini Dar es salaam.



2



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...