Itel kutikisa soko la smartphone ikishirikiana na  msanii mkubwa Afrika 

KAMPUNI ya simu za mkononi ya itel inaeleza kuwa mwezi Aprili kampuni hiyo itazindua rasmi simu mpya ambayo itakwenda sambamba na kumtangaza balozi wake wa itel  kwa mwaka 2021.

Ingawa taarifa hizi hazijathibitishwa rasmi, kuna  chanzo ndani ya kamunii hiyo ambacho kimedokezea taarifa hizi.

“Mwezi Aprili itel imejiandaa kuzindua rasmi simu yake mpya toleo la A’series lakini kikubwa ni kwamba tutamtangaza balozi wetu wa itel kwa mwaka 2021, balozi huyu ni msanii mkubwa sana Afrika” kimedokeza chanzo hicho.

Pamoja na kutotaja jina la msanii huyo,katika kurasa za itel za Instagram na Facebook  imeelezwa kuwa balozi huuyo ni msanii wa muziki aina ya afro beat, afro pop na bongo flava pia.

                           indextyu.jpg

Moja ya post za itel ukurasa wa instagram iliyokuwa ikiwataka wafuasi  wake kutabiri ni msanii gani.

Simu hiyo itakayozinduliwa na msanii huyo ambaye jina lake bado halijatajwa, ni simu yenye fasheni ya waterdrop na plus na ni full screen. Simu hiyo itakayouzwa kwa bei nafuu inatarajiwa kusambazwa nchi nzima katika maduka ya simu.

index12.jpg

Hii ni miongoni mwa post kutoka ukurasa wa itel Tanzania Instagram iliyoelezea kuwa msanii huyo anajihusisha na sanaa ya muziki aina ya afro beat, afro pop na bongo flava.

Ikumbukwe kuwa  itel Tanzania  imewahi kuwa na balozi ambaye ni mwigizaji wa bongo muvi Bi. Irene Uwoya na kushirikiana naye katika kunadi bidhaa zake mwaka 2017. Je, safari hii ni nani anayezungumziwa katika minong’ono inayoendelea?

Ili kujua nani ni nani, yupi atakuwa balozi wa itel  na atatangazwa lini, fuatilia taarifa zetu hapa tutaendelea kukujuza na pia unaweza kufuatilia kurasa za itel Instagram, Facebook na twitter  kwa jina la itel Tanzania au bofya hapa: https://www.instagram.com/iteltanzania/

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...