Charles James, Michuzi TV

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais-Tamisemi, Selemani Jafo ametoa siku mbili kwa Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Joseph Mafuru kuhakikisha mageti yote ya kituo hiko yako wazi na yanafanya kazi.

Jafo ametoa maagizo hayo leo alipofanya ziara ya kutembelea Kituo hiko, Soko Kuu la Job Ndugai na eneo la mapumziko la Chinangali miradi ambayo ilijengwa kwa pamoja.

Akizungumza na viongozi wa Mkoa na Jiji la Dodoma, Waziri Jafo amesema miradi hiyo ya Stendi na Soko imegharimu kiasi kikubwa cha fedha hivyo ni vema Jiji la Dodoma liwe na mipango mizuri ya kuiendesha.

Ameelezwa kukerwa na uendeshaji wa Soko la Ndugai ambalo licha ya kujengwa kwa fedha nyingi bado halionekani kuwa na wafanyabiashara wengi na hivyo kulitaka jiji hilo kubuni mikakati ya kuvutia wananchi kwenda kufanya biashara kwenye soko hilo.

Waziri Jafo pia ameitaka Kampuni ya Ulinzi ya Suma JKT ambayo ndio wasimamizi wa ulinzi wa kituo hiko kuacha tabia ya kuwabughudhi na kuwanyanyasa wafanyakazi wa Idara nyingine ambazo ziko ndani ya kituo hiko.

" Nitoe pongezi kwa uongozi wa Mkoa na Wilaya kwenye suala la Usafi hapa kituoni mmejitahidi sana lakini pia niwaase ndugu zetu wa Suma JKT kuzingatia utu wanapotoa huduma za ulinzi KWA watu ambao ni watumishi wa kituo hiki," Amesema Jafo.

Waziri Jafo pia ameagiza kuwepo kwa vitambulisho kwa wafanyakazi wa idara zote zinazotoa huduma ndani ya stendi hiyo ili kuepusha malalamiko yanayotolewa kwa Suma JKT.

" Eneo hili likiwa bize hakuna mfanyabiashara atataka kuacha kibanda chake wazi, mzunguko utakuepo, fanyeni utaratibu wa kukutana na wadau wa stendi hli kuhakikisha mnapunguza kero zilizopo

Kituo hiki kikiwa bize watu watapata huduma za usafiri lkini pia kuna watu watapata fedha," niwapongeze stendi kuwa safi lakini bado jitihada zinahitajika kuvutia wafanyabiashara kuja kufanya biashara zao hapa," Amesema Jafo.







 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...