Na Said Mwishehe, Michuzi TV
KAMPUNI
ya Mafuta ya Puma Tanzania ambayo ni namba moja katika biashara ya
mafuta imeungana imeungana na wanawake wote duniania katika kuadhimisha
siku ya kimataifa ya mwanamke inayo adhimishwa tarehe 8 Machi kila mwaka
huku ikieleza kwamba inatambua na kuthamini mchango wa makundi yote ya
wanawake nchini katika kushiriki katika shughuli za ujenzi wa Taifa
letu.
Aidha kampuni hiyo kwa kutambua umuhimu wa siku ya Wanawake
Duniani , pamoja na mchango wao imeamua kuitumia siku ya leo pamoja na
mambo mengine kutoa zawadi ya mafuta kwa wanawake katika makundi
mbalimbali wakiwemo wanawake viongozi, mashuhuri pamoja na wanawake
wajasiriamali wadogowadogo walioko kwenye maeneo mbalimbali.
Wakizungumza
wakati wa kuadhimisha siku hiyo na baada ya kutoa zawadi ya mafuta kwa
wanawake wa makundi mbalimbali wakiwemo wanawake wanaondesha Bajaji kwa
ajili ya kujitafutia riziki, maofisa wa kampuni kwa nyakati tofauti
wameeleza kwamba kwa kutambua umuhimu wa Wanawake kwenye jamii ya
kitanzania na wakiwa msatari wa mbele kusheherekea mafanikio ya wanawake
walioko nchini, kampuni ya Puma Energy Tanzania Limited imeamua
kuadhimisha siku hiyo kwa kuwatambua baadhi ya wanawake wa kupigiwa
mfano kwenye jamii yetu na kuwazawadia full tank ya mafuta kwenye
magari yao pamoja bajaji.
Akielezea zaidi baada ya kuwazawadia
mafuta wanawake hao wakupigiwa mfano iliyo fanyika katika kituo cha
Mafuta cha Puma Upanga, Meneja wa Operations wa Kampuni Lameck Hiliyai
amesisitizia Puma Energy Tanzania inathamini mchango wa wanawake katika
kampuni na katika jamii na inafanya kila jitihada kuhakikisha kunakuwa
na uwiano unaoridhisha wa wanawake na wanaume katika kampuni.
Aidha,
amewahamasisha wanawake kujitokeza zaidi kushiriki katika shughuli
mbalimbali katika biashara ya mafuta na kuachana na kasumba zilizo
zoeleka kwamba hizi ni shughuli za wanaume na kwamba kampuni hiyo
ambayo ni namba moja Tanzania katika biashara ya mafuta ni wajibu wao
kuendelea kuboresha hali za wafanyakazi wao wanawake lakini zaidi
wanawake katika jamii mbalimbali zinazowazunguka.
Awali Meneja
wa Rasilimali watu wa Puma Energy kwa bara Afrika Loveness Hoyange
alieleza kuwa kampuni hiyo inatambua namna wanawake hao wanavyocharika
katika harakati za ujenzi wa taifa. "Tunatambua namna gani wanawake siku
hizi wanajituma, mfano hawa wenye ulemavu hawajachukulia hali yao kuwa
sababu ya kujibweteka wanafanya kazi inayowawezesha kuendesha maisha".
Ameongeza
kwa kuliona hilo, kampuni yao imeamua kuwapatia mafuta ili nao waweze
kusherehekea siku hii ya wanawake kwa pamoja huku akisisitiza wanatambua
mchango wao katika sekta ya usafirishaji.
Kwa upande wake
mwanamama Jasimin Milanzi mwenye ulemavu wa viungo ambaye
anajishughulisha na utoaji huduma ya kusafirisha abiria kwa kutumia
usafiri wa bajaji, amesema anajisikia fahari kuwa miongoni mwa wanawake
ambao wamepata zawadi ya kujaziwa mafuta na kampuni hiyo na
imedhihirisha kumbe nao mchango wao kwenye jamii unatambulika huku
akisisitiza licha ya kwamba ni walemavu wa viungo lakini wana akili kama
walivyo binadamu wengine.
Msanii maarufu nchini katika Muziki wa bongofleva Judith Wambura a.k.a Lady J Dee katikati akishuhudia gari yake ikijazwa Mafuta ikiwa ni zawadi kutoka Kampuni ya Mafuta ya Puma Tanzania ikiwa ni sehemu ya kampuni hiyo kutambua mchango wa Wanawake wa Kada mbalimbali katika maendeleo ya nchi yetu katika kuadhimisha siku ya Wanawake Duniani iliyoadhimishwa jana Machi 8,2021.
Mwanadada maarufu katika anga ya muziki wa kizazi kipya Judith Wambura a.k.a Lady Jay Dee akitoa shukurani kwa Kampuni ya Mafuta ya Puma Tanzania kwa zawadi ya Mafuta waliompa kama sehemu ya kutambua mchango wake na mchango wa Wanawake wengine wote katika kuleta Maendeleo nchini.Zawadi hiyo inakwenda sambamba na maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani ambayo huadhimishwa kila ifikapo Machi 8 ya kila Mwaka
Msanii
maarufu nchini katika Muziki wa bongofleva Judith Wambura a.k.a Lady Jay Dee
katikati akiwa na Wafanyakazi wa Kampuni ya Mafuta ya Puma Tanzania baada ya
kumkabidhi zawadi ya kumjazia mafuta ‘full tank’ kwenye gari yake na zawadi
ndogo,ikiwa ni sehemu ya kampuni hiyo kutambua mchango wa Wanawake wa Kada
mbalimbali katika maendeleo ya nchi yetu katika kuadhimisha siku ya Wanawake
Duniani iliyoadhimishwa jana Machi 8,2021.
Wafanyakazi wa Kampuni ya Mafuta ya Puma Tanzania wakiwa na Mwanamama Mwenye ulemavu wa viungo Bi.Jasmine Milanzi anaejishughulisha na utoaji wa huduma ya usafiri mkoani Dar es Salaam kwa kutumia Bajaji yake alipokuwa akijaziwa mafuta na kampuni hiyo kama zawadi kwa Wanawake katika kuadhimisha siku ya Wanawake Duniani iliyoadhimishwa jana Machi 8,2021.
Wanawake
wenye Ulemavu wa Viungo wanaojishughulisha na utoaji huduma ya kusafirisha
abiria kwa Bajaji mkoani Dar es Salaam wakiwa katika picha ya pamoja na Wafanyakazi
wa Kampuni ya Mafuta ya Puma Tanzania mara baada ya kujaziwa mafuta kwenye
Bajaji zao ikiwa ni zawadi kwa Wanawake wote nchini katika kuadhimisha siku ya
Wanawake Duniani iliyoadhimishwa jana Machi 8,2021.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...