Baadhi ya mafuvu ya vichwa ya wanyama yakiwa katika moja ya banda la vivutio vya utalii na uhifadhi lililopo kwenye tamasha la Kisarawe Ushoroba Festival

Meneja wa Vodacom Tanzania Foundation Sandra Oswald akizungumza kwenye Tamasha la Kisarawe Ushoroba Festival linalofanyika katika viwanja vya shule ya Chanzige wilayani Kisarawe ambalo linalolenga kuijulisha jamii vivutio vilivyopo kwenye hifadhi ya msitu wa mazingira asilia wa Kazimzumbwi, tamaduni za Wazaramo pamoja na kutangaza hifadhi mpya ya Taifa ya Mwalim Nyerere.


Mhifadhi Mazingira kutoka WWF, Dkt. Severin Kalonga akielezea jambo kwa Waziri wa TAMISEMI , Seleiman Jafo (kushoto) alipotembelea banda la Vodacom na WWF kwenye maonesho ya Kisarawe Ushoroba Festival. Kulia ni Meneja wa Vodacom Tanzania Foundation, Sandra Oswald

Msanii Aunt Ezekiel(wa tatu kushoto) akiwa na wasanii wenzie wakiingia kwenye viwanja cha Chanzige ambako tamasha la Kisarawe Ushoroba Festival linaendelea.




Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo(katikati) akiwa na wasanii mbalimbali pamoja na wananchi wakicheza ngoma ya asili ya kabila la Wazaramo.
 

Sehemu ya wapiga ngoma ya asili za Kizaramo wakijiandaa kupiga ngoma zao ili kutoa burudani kwa wageni waalikwa wakati wa tamasha la Kisarawe Ushoroba Festival. 


Na Said Mwishehe, Michuzi TV

KAMPUNI ya Vodacom Tanzania kupitia asasi yake ya Vodacom Tanzania Foundation imedhamini Tamasha la Kisarawe Ushoroba Festival linalofanyika wilayani Kisarawe kwa siku tatu mfululizo.

Tamasha hilo linalenga kuwajulisha watalii kuhusu vivutio vilivyopo kwenye hifadhi ya msitu wa mazingira asilia wa Kazimzumbwi, tamaduni za Wazaramo pamoja na kuitangaza hifadhi mpya ya Taifa ya Mwalim  Nyerere. Pia tamasha hilo litaambatana na mbio za marathon zitakazofanyika Jumapili ya wiki hii .

Akizungumza kuhusu tamasha hilo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Seleman Jafo amesema tamasha la Kisarawe Ushoroba Festival pamoja na mambo mengine litasaidia kuleta Kisarawe mpya kwa kutangaza vivutio vilivyopo na kujua asili ya wazaramo.

"Kwa kuzingatia hilo litasaidia pia kuifanya wilaya hiyo kuwa ushoroba kwa watalii kuelekea kuona hifadhi ya Taifa ya Mwl. Nyerere iliyopo wilayani  Rufiji,"amesisitiza Jafo huku akitumia nafasi hiyo kuendelea kumpongeza Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo kuwa mbunifu kwa kuanzisha tamasha hilo kubwa na lenye tija kwa taifa ili kuhamasisha watalii kutembelea hifadhi ya Taifa ya Mwl. Nyerere.

Kwa upande wake Jokate amesisitiza kupitia tamasha hilo wanaamini wananchi wengi watafika kuitembelea Kisarawe na kushuhudia vivutio vya utalii ambavyo wamejaaliwa kuwa navyo, lakini pia kupitia Kisarawe Ushoroba Festival wanahamasisha watu kuwekeza ndani ya wilaya hiyo.

 "Tuna maeneo mengi ambayo mtu anaweza kuja kuwekeza , sote tunafahamu Kisarawe ndio ushoroba(njia) kuelekea Hifadhi ya Taifa ya Mwalim Nyerere na baada ya Rais kuizindua hifadhi hiyo pia ameweka wazi barabara hii inayopita Kisarawe kwenda katika hifadhi hiyo itajengwa kwa kiwango cha lami.

 "Hii ni fursa kwetu wananchi wa Kisarawe na ndio maana tunawaambia watu wenye uwezo wa kuwekeza waje, tunawakaribisha na tunaamini kabla ya mtalii kwenda Hifadhi ya Taifa ya Mwalim Nyerere basi kwanza anapotoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere atapita hapa kwetu."

Awali Meneja wa Vodacom Tanzania Foundation, Sandra Oswald akizungumza kwenye mkutano huo  alisema wao kama wadau wakubwa wa mazingira wanafarijika kuwa sehemu ya tamasha hilo la mazingira na utalii kwa wilaya ya Kisarawe.

"Sisi kama wadau sio mara ya kwanza kutoa ushirikiano wetu kwenye mazingira,  tulishawahi kufanya hivyo mkoani Dodoma kwenye " Kijanisha Dodoma "kwa kupanda miti mkoani humo,"amesema Sandra.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...