BENKI kuu ya Tanzania (BoT,) imefikia uamuzi wa kuhamisha mali na madeni yote ya Benki ya China Commercial Bank Limited kwenda kwa benki ya NMB Bank PLC baada ya kubaini upungufu wa mtaji kinyume na matakwa ya sheria.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Mkoani Dar es Salaam Gavana wa Benki Kuu (BoT) Prof. Florens Luoga amesema, Benki Kuu ikiwa na jukumu la kusimamia sekta ya fedha  Novemba 19, 2020  iliiweka Benki hiyo chini ya usimamizi wake pamoja na kusitisha shughuli za utoaji wa huduma za kibenki kwa benki ya China Commercial Bank kwa siku 90 ili waweze kufanya tathimini na kuchukua hatua zaidi.

Amesema, kabla ya kuiweka benki hiyo chini ya usimamizi BoT ilifanya jitihada kadhaa kupitia wamiliki, bodi za Wakurugenzi na menejimenti kwa kuwataka kuongeza mtaji ili kufikia kiwango kinachohitajika kisheria na licha na ya kupewa muda wa kutimiza matakwa hayo jitihada hazikufanikiwa.

Amesema, China Commercial Bank ilipewa leseni na kuanza shughuli za kibenki nchini mwaka 2015 na kuwa moja ya Benki zenye ukuaji wa chini na kusababisha hasara kwenye biashara kwa muda wote tangu ianze kutoa huduma za kibenki na hadi kuchukuliwa na BoT Benki hiyo ilikuwa na mali zisizozidi shilingi bilioni 5 na ilikuwa na tawi moja pekee Mkoani Dar es Salaam.

Amesema kwa sasa BoT,  NMB PLC na wadau wengine wanaendelea kuandaa taratibu za kisheria za kukamilisha mchakato wa uhamishaji wa mali na madeni ya China Commercial Bank Limited kwenda NMB BANK PLC.

Vilevile amesema, wateja wenye amana na wadai wa China Commercial Bank watapewa taarifa ya tarehe ya kuanza kupata huduma za kibenki kupitia NMB PLC na wateja wenye mikopo wanatakiwa kuendelea kulipa mikopo yao kwa mujibu ya mikataba yao.

Pia amewahakikishia watanzania kuwa BoT itaendelea kulinda maslahi ya wateja wenye amana katika mabenki kwa utulivu na ustawi katika sekta ya fedha.

Gavana wa Benki Kuu (BoT) Prof. Florens Luoga pamoja na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB,Bi Ruth Zaipuna wakionesha nyaraka za uamuzi wa kuhamisha mali na madeni yote ya Benki ya China Commercial Bank Limited kwenda kwa benki ya NMB Bank PLC baada ya kubaini upungufu wa mtaji kinyume na matakwa ya sheria
Gavana wa Benki Kuu (BoT) Prof. Florens Luoga pamoja na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB,Bi Ruth Zaipuna wakikabidhiana nyaraka za uamuzi wa kuhamisha mali na madeni yote ya Benki ya China Commercial Bank Limited kwenda kwa benki ya NMB Bank PLC baada ya kubaini upungufu wa mtaji kinyume na matakwa ya sheria
Gavana wa Benki Kuu (BoT) Prof. Florens Luoga pamoja na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB,Bi Ruth Zaipuna wakisaini nyaraka za uamuzi wa kuhamisha mali na madeni yote ya Benki ya China Commercial Bank Limited kwenda kwa benki ya NMB Bank PLC baada ya kubaini upungufu wa mtaji kinyume na matakwa ya sheria

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...