Jane Edward, Michuzi TV, Arusha

MBUNGE wa Viti Maalumu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Arusha, Zaituni Swai ,amewataka wanafunzi wa shule za sekondari na msingi mkoani humo , kutumia nafasi ya elimu waliopata kusoma ili kufikia malengo ya maisha yao ya baadae baada ya kuhitimu masomo.

Mbunge , aliyasema hayo wakati wa ziara yake ya kikazi wilayani Arumeru, alipotembelea shule ya sekondari ya Maji ya Chai ambapo aliotesha miti 100 kwenye shule hiyo, kwa ajili ya kutunza mazingira ya eneo hilo.

Alisema serikali imejitahidi kuboresha miundombinu ya elimu ili kutoa fursa kwa wanafunzi kusoma katika mazingira bora na wezeshi ya kujifunzia ili kuongeza chachu kwa wanafunzi kusoma na kufikia malengo.

“Serikali inatoa fedha nyingi kwa ajili ya kuboresha sekta ya elimu nchini, ili kutoa fursa kwa wanafunzi wote kusoma katika mazingira bora na wezeshi, lengo la serikali kufanya hivyo ni kuwasaidia wanafunzia kusoma kwa bidii ili kufikia malengo waliyojiwekea katika maisha yao ya baadae baada ya kuhitimu masomo yao,”alisema Zaituni.

Hata hivyo, alisema katika kuboresha sekta ya elimu nchini, serikali imetoa elimu bure hivyo mpango huo umeongeza chachu kwa wanafunzi kusoma na kuongeza kiwango cha ufaulu.

Vile vile katika ziara hiyo, wilayani humo,Zaituni, alishiriki katika ujenzi wa jengo la mradi wa mashine ya kusanga la Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Meru(UWT), na alichangia vifaa vya umeme na mifuko ya saruju kwa ajili ya kukamilisha ujenzi huo.

Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Maji ya Chai,Titus Kadanda, licha ya kumshukuru  mbunge huyo, kutembelea shule hiyo, alisema shule hiyo inakabiliwa na tatizo la upungufu wa vyumba vya madarasa na mada 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...