MFUMUKO wa Bei wa Taifa  kwa Mwaka ulioishia mwezi Februari 2021 umepungua kutoka asilimia 3.5 kwa Mwaka ulioishia mwezi Januari ,2021 hadi kufikia asilimia 3.3 kwa mwaka ulioishia mwezi Februari,2021.

 

Akizungumza na waandishi wa habari jana Jijini Dodoma Kaimu Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii Ruth Minja kuwa inamanisha kuwa Kasim ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa Mwaka iliojishika mwezi Februari 2021 umepungua ikiliganushwa na kasi iliyokuwepo kwa Mwaka iliojishika mwezi Januari 2021.

 

Aidha alisema Kupungua kwa mfumuko wa Bei kwa mwaka ulioishia mwezi Februari 2021 umechangiwa hasa nakupungua kwa bei za Baadhi ya bidhaa zisizo za vyakula kwa kipindi kikichoishia Februari 2021 zikilinganishwa na bei za mwezi Februari 2020.

 

Alisema Baadhi ya bidhaa zisizo za vyakula zilizopungua bei kwa mwezi Februari 2021 zikilinganishwa na bei za Mwezi Februari 2020 nipamoja na Thamani,kwa asilimia 5.3, Mafuta ya taa kwa asilimia 15.7 ,Vifaa vya nyumbani kama vile pasi ya umeme kwa asilimia 4.7, vyomboa vya ndani kwa asilimia 3.3 Dezeli kwa asilimia 22.8,Petroli kwa asilimia 13.4.


Hata hivyo alisema mfumuko wa bidhaa za vyakula na vinjwaji baridi kwa mwezi Februari 2021 umeongezeka kutoka asilimia 2.8 mwezi Januari  2020 hadi asilimia 3.6.

 

Kuhusu  hali ya mfumuko wa Bei kwa nchi za Afrika Mashariki kwa Mwaka ulioishia mwezi Februari 2021  Minja amebainisha kuwa Nchini Kenya mfumuko wa Bei kwa mwaka ulioishia mwezi Februari 2021 umeongezeka kutoka asilimia 5.69 kwa mwaka ulioishia mwezi Januari 2021 hadi kufikia asilimia 5.78 kwa mwaka ulioishia mwezi Februari 2021 .


Kuwa nchini  uganda mfumuko wa Bei kwa mwaka ulioishia mwezi Februari 2021 umeongezeka kutoka asilimia 3.7 kwa mwaka ulioishia mwezi Januari 2021 hadi kufikia asilimia 3.8.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...