Na Shukrani Kawogo, Njombe.

Wafanyabiashara wilayani Ludewa mkoani Njombe wameiomba serikali kuharakisha ujenzi wa miundombinu ya barabara zinazounganisha mikoa na wilaya za jirani ili kuweza kutumia fursa mbalimbali za kibiashara ambazo zitawaingizia kipato na kukuza uchumi wa wilaya hiyo na taifa kwa ujumla.

Hayo wameyasema katika mkutano wa wafanyabiashara pamoja na mbunge wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga uliofanyika wilayani humo kwa lengo la kusikiliza changamoto mbalimbali zinazowakabili na kuzitafutia ufumbuzi.

Akizungumza katika mkuitano huo mmoja wa wafanyabiashara hao Flovin Mtitu amesema wamekuwa wakipata tabu sana katika kupata bidhaa zinazotoka mkoa wa Ruvuma hasa saruji ya Dangote inayotokea mkoani Mtwara ambapo wanalazimika kuzunguka mpaka Njombe mjini ndipo waje wilaya ya Ludewa kitu ambacho kinawapa gharama kubwa sana.

Amesema endapo daraja la Ruhuhu lingemalizika mapema lingeweza kuwasaidia kupata bidhaa hizo kwa urahisi au serikali ijenge daraja katika kijiji cha Masimavalafu ambacho kinapakana na mkoa wa Ruvuma ambako huko ni rahisi zaidi kuliko Ruhuhu na Njombe na ingeweza kuwapunguzia gharama za usafirishaji wa bidhaa.


"Ukipita Ruhuhu uje uikute Mbinga  itapunguza gharama kidogo lakini bado na ukisema upite Mavanga nako ni gharama hivyo mimi nashauri njia rahisi zaidi itakayoweza kuwa msaada kwa wafanyabiashara na itakayoleta muingiliano wa watu katika wilaya yetu na kukuza uchumi kwani pikipiki zitakuwa na uwezo wa kwenda na kurudi nashauri tujenge daraja Masimavalafu na tutapata matokeo mazuri", Alisema Mtitu.

Naye Anosiata Lugome ni mfanyabiashara wa mazao ya chakula wilayani humo amemuomba mbunge huyo kuwatafutia soko la uhakika la mazao hayo kwani hali waliyonayo ni mbaya kiuchumi kwakuwa wamekuwa wakitumia gharama nyingi kwa kilimo halafu matokeo ya biashara baada ya mavuno yamekuwa si rafiki kwao kwani mapaka sasa mahidi yapo chini sana ambapo yanauzwa debe elfu tano.

Ameongeza kuwa miaka ya nyuma wanunuzi "FOOD" walikuwa wanaweka  kituo cha ununuzi wa mahindi na wananchi walikuwa wanapata fursa ya kuuza mahindi yao pale lakini kwa sasa hicho kitu hakuna.

Wile Mhagama ni miongoni wa wafanyabiasha hao ambapo amezungumzia kero kubwa wanayoipata kutoka kwa Mamlaka ya Mapato (TRA) ambapo amesema TRA wamekuwa wakiwaongezea kodi kila mwaka pasipo kuwa na sababu za msingi na kufanya biashara zao kudhohofika hivyo wanaiomba serikali kufanya makadilio ya kodi ambayo watakubaliana kulipa kwa kipindi chote.

"Hali tuliyonayo wafanyabiasha ni mbaya sana na watu wa TRA wamekuja kuongeza ubaya zaidi, hizi mashine zao zinaonyesha mapato ya mwaka mzima tena unakuta kila mwaka yanalingana tu lakini utashangaa unaambiwa unatakiwa uongeze kodi ukimuuliza sababu anakwambia kwa kipata chako hukustahili kulipa kiwango hiki, sasa kama sistahili kwanini mliniambia nilipe hiki? utasikia nilikuonea huruma tu! sasa kama kipindi kile ulinionea huruma sasa hivi huyo huruma amekwenda wapi?" Alisema Mhagama.

Aidha kwa upande wa mbunge wa jimbo hilo amezungumzia hatua mbalimbali alizochukua katika kuhakikisha miundombinu ya barabara inafanikiwa ambapo amesema juu ya ujenzi wa daraja la Simavarafu kutokea Ruvuma tayari alishaanza mchakato wake ambapo tayari alishaongea na mbunge wa Mbinga vijijini pamoja na diwani wa kule na wamekubaliana kukutana jijini Dododa sambamba na diwani wa Ibumi kujadili.

Amesema lengo lao hasa ni kupata kivuko ambapo wataiomba serikali iwasaidie kupata kivuko hicho ambapo kama itashindikana kupata kivuko kipya basi wawape hata kivuko kama kitatolewa kutoka sehemu nyingine ili waanze kutumia wakati michkato mingine ikiendelea.

"Nimefanikiwa kupata andiko la mradi huo ambalo liliandaliwa kati ya mwaka 2004 hadi 2005 na mwandishi anaitwa Mtabiru kwahiyo suala hili tutahakikisha tunalifanyia kazi baada ya bunge la bajeti kuisha sisi wabunge tutakaa kwa pamoja na madiwani wetu ili kuona tunaanzia wapi katika ufuatiliaji", Alisema Kamonga.

Sanjari na hayo pia alisema mawazo yote yaliyotolewa na wafanyabiashara hao ameyapokea na kuhusu ununuzi wa mahindi tayari yupo kwenye mchakato wa kuona uwezekano wa kuwasaidia.

Mbunge wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga akizungumza na wafanyabiashara wilayani humo kujadili changamoto mbalimbali zinazowakabili
Baadhi ya wafanyabiashara wa wilaya ya Ludewa wakifuatilia mjadala wa kujadili changamoto zao uliokuwa ikiendelea sambamba na mbunge wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga.


Baadhi ya viongozi ngazi ya kata na wilaya wakisikiza changamoto za wafanyabiashara wilayani Ludewa.
Mmoja wa wafanyabiashara wilayani Ludewa Anosiata Lugome akitoa changamoto ya bei ya mahindi wilayani humo mbela ya mbunge wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga pamoja na Viongozi wa CCM wilaya (hawapo pichani)

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...