:Baadhi ya vifaa vya umeme vya mradi uliotelekezwa wilayani Ludewa kama vilivyokutwa na mpiga picha wakati wa ziara ya mbunge wa Ludewa.


 

Na Amiri Kilagalila,Njombe

Wananchi wa kata ya Kilondo tarafa ya Mwambao wilayani Ludewa mkoani Njombe wameilalamikia serikali kwa kushindwa kukamilisha utekelezaji wa mradi wa umeme kupitia maporomoko ya maji ya mto Kilondo ulionza utekelezwaji mwaka 2015 na kuishia njiani kutokana na changamoto mbali mbali.

Alto Mwakila na Josephat Mwandesele wakizungumza wilayani humo katika mkutano wa mbunge wao wameiomba serikali kuangalia mradi huo upya kwa kuwa ndio tegemeo lao la pekee kwa sasa katika ndoto za kupata nishati ili kuinua uchumi wa kata za tarafa hiyo uliodumaa kwa kukosa miundombinu ya nishati na barabara.

“Wananchi bado tunashauku na huu mradi tunaiomba serikali iliangalie hili kwa jicho la huruma kwasababubu tunashida ya umeme”alisea Josephat Mwandesele

“Siku nyingi tunausubiri huu mradi lakini bado haukamiliki hili ni changamoto kidogo na sisi kwenye vijiji vyetu hatuna kabisa umeme kwa hiyo tunao serikali itupe nguvu ili mradi huu uweze kukamilika”alisema Alto Mwakila

Laulent Kiunga ni mwenyekiti wa kijiji cha Kilondo amesema mradi huo unaosimamiwa na REA umekwama kutokana na sababu mbali mbali na vifaa vikiwa vimefika huku huku afisa tarafa wa tarafa ya Mwambao Linus Malamba,akibainisha kuwa mradi huo ni mkubwa kwenye wilaya ya Ludewa utakaoleta faida kwa wananchi wa kata za Kilondo,Lumbila,Ikombe,Matema na kasha kuingizwa kwenye Glidi ya taifa.

Naye Felix Mwakila diwani wa kata ya Kilondo amesema baadhi ya shughuli zimeshafanyika ikiwemo usogezwaji wa vifaa,ununuzi wa mashine,ujenzi wa banio ambao umeishia njiani pamoja na nyumba ya motor lakini fedha za kukamilisha mradi zimekwama.

“Kwa hiyo wananchi wanahitaji kunufaika kutokana na mradi huu uliopo na malengo ya wananchi ni kuona umeme unawake kama unavyojua umeme ni maendeleo,tuiombe serikali inusuru wananchi kwa kuwa wanafika wakati wanakata tama na mradi”alisema Felix Mwakila

Kwa upande wake mbunge wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga amesema kwa kuwa juhudi za ujenzi wa miundombinu zilishaanza ataendelea kuishauri serikali kukamilisha mradi huo huku hatua za awali zikiwa zimechukuliwa kwa kuwasiliana na REA ili kufanikisha mradi.

“Niliwaomba watu wa REA na walikuja hapa na kuchukua changamoto zote na ni imani yangu kwamba kwenye bajeti hii sasa wataingiza mradi huu kama kipaumbele ili wananchi wa Kilondo nao waweze kupata umeme wa uhakika”alisema Kamonga

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na viongozi wa serikali ya kata,milioni 196 fedha iliyotolewa na serikali imekwisha tumika katika shughuli za mradi huo huku  mkandarasi akiwa ameomba milioni 300 kwa ajili kukamilisha mradi utakaozalisha zaidi ya Megawati 25.

Mbunge wa Ludewa Joseph Kamonga akizungumza mara baada ya kutembelea eneo la ujenzi wa mradi wa umeme kupitia maji yam to Kilondo uliopo tarafa ya Mwambao.
Baadhi ya wananchi wa kata ya Kilondo wakati wakitoa hoja na kumpa changamoto ya umeme na mradi mbunge wa Ludewa alipowatembelea katika kata yao.

Baadhi ya wananchi wa kata ya Kilondo wakati wakitoa hoja na kumpa changamoto ya umeme na mradi mbunge wa Ludewa alipowatembelea katika kata yao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...