Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV

KARNE za sasa Klabu ya Simba imeendelea kulitawala Soka la Tanzania si kwa Wanaume, si kwa Wanawake, sehemu mbalimbali Simba imeendelea kuinyanyasa Yanga, si kwenye uongozi si kwenye matokeo ya uwanjani kote Yanga imeonyesha udhaifu kuzidiwa na Simba.


SOKA LA WANAWAKE

March 5, 2021 Timu za Wanawake za Simba na Yanga zilikutana kwenye Ligi Kuu ya Wanawake ya Tanzania, mchezo uliopigwa kwenye dimba la Uhuru, Dar es Salaam, katika mchezo huo Simba Queens iliibuka kidedea kwa ushindi wa bao 3-0 dhidi ya Yanga Princess.


Simba Queens imeendelea kuongoza Ligi hiyo kwa kuwa na alama 39 na kucheza michezo yake yote bila kufungwa (Unbeaten) wakiishusha kileleni Yanga Princess katika nafasi ya kwanza wakibaki na alama zao 38 huku wakipoteza mchezo huo pekee katika Ligi hiyo.


Mabao ya Simba Queens katika mchezo huo yalifungwa na Mwanahamisi Omar ‘Gaucho’ dakika ya 29, bao la pili likifungwa na Opah Clement kwa mkwaju wa Penalti dakika ya 43 na Joell Bukuru dakika ya 50.

Kwa matokeo hayo, Simba Queens imeenda kukaa kileleni mwa msimamo wa Ligi hiyo ya Wanawake kwa alama hizo 39 na michezo 15 wakati Yanga Queens wakiwa nafasi ya pili wenye alama 38 na michezo 15.


SOKA LA WANAUME

Yanga SC walicheza michezo yao bila kufungwa (Unbeaten) katika Ligi Kuu Soka Tanzania Bara upande wa Wanaume, lakini waliruhusu kufungwa na Coastal Union, Wagosi wa Kaya wakipata ushindi wa bao 2-1 katika dimba la Mkwakwani, jijini Tanga hiyo ikiwa ni mchezo wa kwanza wa Yanga SC kupoteza katika Ligi Kuu.

Simba SC wakiwa kwenye michezo ya Kimataifa bado wana viporo katika Ligi hiyo na endapo watashinda viporo hivyo, Simba SC watashika usukani na kuongoza Ligi Kuu Soka Tanzania na kunyakua ubingwa endapo Ligi hiyo itaisha kwa Simba SC kuongoza msimamo.

Licha ya kupoteza michezo yake miwili ya Ligi Kuu, Simba SC inapewa nafasi kubwa kutwaa Taji la Ligi Kuu Soka Tanzania Bara (VPL) msimu huu na taji la Kombe la Shirikisho (ASFC) ijapokuwa lolote linaweza kutokea katika mpira wa miguu.


UONGOZI WA TIMU ZOTE MBILI

Simba SC wameendelea kufanya vizuri kipindi hiki kutokana na Uongozi imara wa Klabu hiyo ukiongozwa na Afisa Mtendaji Mkuu, Mwanadada Barbara Gonzalez sambamba na Mwekezaji wa Klabu, Mohamed Dewji (MO) hii inaweza kuwa chachu ya Wachezaji na Benchi zima la ufundi kufanya vizuri katika michezo yao yote ya ndani na Kimataifa.

Yanga SC wao wapo katika harakati za mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji wa Klabu, suala ambalo hata Simba SC bado hawajalikamilisha kisawa sawa.

Licha ya ufadhili wa Kampuni ya GSM Klabuni hapo, bado Wanachama, Mashabiki wa Yanga SC hawajaridhishwa na viwango vya baadhi ya Wachezaji na matokeo yanayopatikana hivi karibuni katia Kikosi hicho cha Mabingwa wa Kihistoria.


USAJILI WA TIMU ZOTE

Simba SC muda wote wamekuwa wakiimarisha Kikosi chao, wengi tumeona kila mchezaji akiifunga Simba bado lazima atasajiliwa kuongeza nguvu, angalia kwa kina Medie Kagere, Luis Jose Miquissone, Bernard Morrison na hata Perfect Chikwende wote waliifunga Simba SC kwa nyakati tofauti na kusajiliwa kikosini hapo.

Yanga SC wamefanya usajiliwa baadhi ya Wachezaji wazuri wakiwemo kina Mukoko Tunombe, Tuisila Kisinda kutoka AS Vita Club ya DR Congo, kina Farid Mussa na wengine wengi kina Michael Sarpong bado imeonekana kushindwa kufua dafu mbele ya Simba SC.

Licha ya kumleta Mshauri wa Klabu, Senzo Mbatha aliyekuwa Simba SC bado Yanga SC hawana imani na Kikosi chao kutwaa ubingwa wa VPL kutokana na mwenendo wa matokeo yao kwa sasa.



 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...