Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Patrobas Katambi (katikati) akizungumza na Vijana wa Kikundi cha Mshikamano kilichokopeshwa Milioni 40 na Halmashauri ya Kahama wakati wa ziara yake ya kikazi ya kufuatilia utekelezaji wa uwezeshaji wa mkopo wa asilimia 4 inayotolewa kwa vijana kupitia halmashauri zilizopo nchini.

Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Patrobas Katambi akiangalia mageti ambayo yanatengenezwa na Kikundi cha Vijana cha Mshikamano kinachojishughulisha na Uchomeleaji na utengenezaji wa bidhaa za Chuma wakati wa ziara yake ya kikazi ya kufuatilia utekelezaji wa mkopo wa asilimia 4 inayotolewa kwa vijana kupitia halmashauri zilizopo nchini.

Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Patrobas Katambi (kulia) akiangalia mkataba wa kikundi cha Vijana cha Mshikamano kilichokopeshwa Milioni 40 na Halmashauri ya Kahama. Kushoto ni Katibu wa kikundi hicho Bw. Harry Ramadhan.

Mwenyekiti wa Kikundi cha Uchumi Viwanda, Bw. Mogeni Kubalunga (kushoto) akimweleza jambo Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Patrobas Katambi (wa pili kutoka kushoto) alipotembelea kikundi hicho ikiwa ni sehemu ya kufuatilia utekelezaji wa uwezeshaji wa mkopo wa asilimia 4 inayotolewa kwa vijana kupitia halmashauri zilizopo nchini.

Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Patrobas Katambi akiangalia urembo wa gypsum alipotembela kikundi cha Vijana cha Uchumi Viwanda kilichopo eneo la Majengo, Halmashauri ya Kahama ili kujionea shughuli za uzalishajimali za vijana.

Muonekano wa mikanda ya gypsum inayotengenezwa na kikundi cha vijana cha Uchumi Viwanda kilichopo eneo la Majengo, Halmashauri ya Kahama.

Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Patrobas Katambi akiwa ameongozana na Mwenyekiti wa Kikundi cha Vijana cha Jipapanue kinachojishughulisha na shughuli za Ufugaji na kilimo alipotembelea kikundi hicho ikiwa ni sehemu ya kufuatilia utekelezaji wa uwezeshaji wa mkopo wa asilimia 4 inayotolewa kwa vijana kupitia halmashauri zilizopo nchini.

PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU

(KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU)

OWM – KVAU

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...