*Zaidi ya sh.bilioni 3 zilizotakiwa kwenda katika makato ya hifadhi ya jamii zaishia mifukoni ya watu .


Na Chalila Kibuda,Michuzi Blog  Songea

 Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Kundo Andrea  amemtaka Posta Masta Mkuu ajitathimini kwa nafasi yake.

Kundo ameyasema katika ziara za kutembelea mashirika na Taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo baada ya kubaini kuwepo kwa wafanyakazi kukunyanyswa na shirika la Posta na kufanya Shirika hilo kudumaa.

Amesema katika unyanyasaji huo ni pamoja na kukosesha mambo ya msingi kwa makato mbalimbali yanayotakiwa Shirika limekuwa halipeleki.

Mhandisi Kundo amesema kuwa kuna zaidi ya sh.bilioni tatu hazijapelekwa katika mifuko ya hifadhi ya Jamii lakini wafanyakazi wakiwa wamekatwa .

Amesema kutokana na shirika hilo kushindwa kupeleka makato kunashusha wafanyakazi kujituma kwani wakienda kuchungulia makato yao hawaoni kitu chochote.

Aidha amesema kuwa wafanyakazi wanaokuwa na uwezo wa kuhoji na kutaka Shirika hilo lifike mbele wamekuwa wakihamishwa kwenda pembezoni ili wachache waendelee na michezo yao.

"Hatuwezi kuwa na shirika lisilojali rasilamali watu wa huku hukuna mabadiliko yanayoonekana sasa mwisho wao umefika katika Wizara ya Mawasiliano" amesema Mhandisi Kundo.

Hata hivyo amesema kuwa wafanyakazi mizigo ndio wanawafanya madudu makubwa ambayo Shirika kila ukiangalia halioneshi mwanga wa kuweza kutengeneza faida ya kuweza kwenda katika huduma za jamii.

Naibu Waziri amesema kuwa matatizo yanayoonekana katika Shirika la Posta ni ugonjwa wa kudumu ambao hakuna mtu wa kuweza kubadilisha Shirika hilo.

Amesema ofisi za Mikoa haziendani kabisa kwa ajili ya kufanya ushindani wa kibiashara kutokana na udumavu wa mawazo na wenye uwezo katika Shirika kuonekana wanaharibu mipango ya watu.

Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Andrea Kundo akizungumza na wafanyakazi wa Shirika la Posta Mkoa Ruvuma alipofanya ziara katika Mkoa huo.
Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Kundo Andrea akizungumza na wafanyakazi wa Shirika la Posta namna wanavyotoa huduma katika Mkoa wa Ruvuma
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...