Charles James, Michuzi TV

NAIBU Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Chamwino mkoani Dodoma, Deo Ndejembi amesema serikali imekubali kujenga mradi mkubwa wa Maji utakaogharimu Sh Milioni 500 katika Kata ya Dabalo wilayani Chamwino.

Ndejembi ametoa kauli hiyo alipofanya ziara ya kikazi katika Kata za Dabalo, Membe na Segala jimboni kwake ambapo amekutana na viongozi wa Serikali na Chama kwenye Kata hizo na kuwaeleza mafanikio ambayo Jimbo hilo limeyapata ndani ya kipindi cha miezi mitatu toka achaguliwe kuwa Mbunge.

Amesema Tarafa ya Itiso ambayo ndio Kata hizo kubwa tatu zipo imekua na changamoto ya maji kwa muda mrefu na moja ya ahadi zake wakati wa kampeni mwaka ilikua ni kumaliza kero hiyo.

Naibu Waziri Ndejembi amesema tayari Waziri wa Maji, Juma Aweso ameshamuahidi kutoa kiasi hicho cha fedha Sh Milioni 500 kwa ajili ya mradi huo mkubwa wa maji kwenye Kata hiyo ya Dabalo.

" Ndugu zangu wa Chamwino nimekuja kuwashukuru kwa imani yenu kubwa mliyonionesha kwenye uchaguzi mkuu uliopita mimi pamoja na Rais wetu Dk Magufuli, sina cha kuwalipa zaidi ya kuwaletea maendeleo makubwa.

Miezi mitatu toka mnichague tayari Serikali imekubali kuleta mradi mkubwa wa maji hapa Dabalo wenye lengo la kumtua Mama Ndoo, ni mradi ambao utakua msaada pia kwa wananchi wa Segala na Membe," Amesema Ndejembi.

Pia amesema tayari Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Dk Leonard Chamuliho amemuahidi kuanza ujenzi wa daraja la Nzali ambalo kwa kipindi kirefu limekua likileta madhara kwa wananchi hasa pindi ambapo mvua zinaponyeesha kwa wingi na kusababisha maji kujaa na kufunika daraja lililopo.

" Waziri Dk Chamuliho ameahidi na tayari alishampigia simu mbele yangu Mkurugenzi wa TANROADS ili atoe fedha za kuanza ujenzi wa daraja la Nzali ambalo limekua likitutesa kwa muda mrefu," Amesema Ndejembi.

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Deo Ndejembi akikagua miundombinu ya barabara inayojengwa na TANROAD kwenye Jimbo lake la Chamwino mkoani Dodoma.
Mafundi kutoka TANROAD wakiendelea na shughuli za ujenzi wa miundombinu ya barabara kwenye Tarafa ya Itiso Wilayani Chamwino ambapo Mbunge wa Jimbo hilo ni Deo Ndejembi. 

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Chamwino mkoani Dodoma, Deo Ndejembi akizungumza na viongozi wa Serikali na Chama kwenye Kata ya Dabalo jimboni kwake.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...