Meneja uhusiano na Elimu kwa Umma Lulu Mengele akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukabidhi vifaa hivyo katika hospitali ya Rufaa Mwananyamala na kusema Sisi NSSF tunaunga mkono juhudi hizi za Serikali ya Awamu ya Tano, na leo hii Wafanyakazi Wanawake ambao tunawawakilisha Wafanyakazi wenzetu wanawake nchi mzima, tumekuja hapa katika Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala kwa ajili ya kutoa msaada wa vifaa tiba, ambao tumeutoa baada ya kujua uhitaji walionao hapa hospitali.Leo jijini Dar es Salaam.
 
Mganga Mfawidhi wa hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala Dkt. Nkungu Daniel akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kupokea msaada huo ambapo aliushukuru Mfuko wa NSSF kwa msaada wa vifaa tiba hivyo ambavyo walikuwa wanavihitaji kwa ajili ya kuwasaidia wagonjwa mbalimbali wanaopata huduma katika hospitali hiyo. leo Mkoani Dar es Salaam.
 
Mwenyekiti wa wanawake (NSSF,) Vaileth Segeja akizungumza na wanahabari mara baada ya kukabidhi msaada huo ambapo ameeleza changamoto wanazozipitia wananawake na kutoa wito kwa jamii kushiriki katika kuzitatua kutokana na thamani ya mwanamke, pia  aliushukuru uongozi wa NSSF kwa kuwajali na kuwasikiliza  bila kuwabagua kama wanawake na wanafanya kazi zao kwa uhuru na wamekuwa chachu ya maendeleo, leo Mkoani Dar es Salaam.

Wafanyakazi wa NSSF na watumishi kutoka hospitalini ya Rufaa Mwananyamala wakiwa wameshika moja ya shuka mara baada ya makabidhiano, leo Mkoani Dar es Salaam.
 
Wafanyakazi wa NSSF na watumishi kutoka hospitalini ya Rufaa Mwananyamala wakiwa wameshika makasha ya mipira 'Gloves' mara baada ya makabidhiano, leo Mkoani Dar es Salaam.

Wafanyakazi wa NSSF wakiwa wameshika mashuka waliyokabidhi katika hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala , leo Mkoani Dar es Salaam.

 
Wafanyakazi wa NSSF wakiwa wanatandika mashuka waliyokabidhi katika hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala kwa matumizi ya wodi ya wazazi, leo Mkoani Dar es Salaam.

 
Mnufaika wa msaada uliotolewa na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF,) Rose Robert akizungumza na wanahabari mara baada kupokea msaada ambapo amewashukuru NSSF kwa kuweka mazingira salama katika wodi ya wazazi, Leo Mkoani Dar es Salaam.


*****************************

Na Amiri Atick, Michuzi Tv

Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), katika kuelekea kilele cha Siku ya Wanawake Duniani, umetoa msaada wa vifaa tiba ambavyo ni mashuka na mipira ya kujifungulia wanawake katika Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala Mkoani Dar es Salaam


Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukabidhi vifaa hivyo hospitalini hapo Meneja uhusiano na Elimu kwa Umma kutoka NSSF, Lulu Mengele amesema, katika kuadhimisha siku ya mwanamke ulimwenguni Shirika hilo limekuwa likiwashika wanawake mkono kwa namna mbalimbali ili kuonesha thamani na umuhimu wao katika jamii.

Lulu amesema, walifika hospitalini hapo na kuona uhitaji wa mipira (Gloves,) na mashuka na kwa kuona umuhimu wa suala hilo wakaona washiriki kwa kuchangia vifaa hivyo ambavyo ni mashuka na mipira (Gloves,) inayotumika wakati wa kujifungua na vyote kwa pamoja vimegharimu  shilingi milioni nane na laki saba.

Aidha amesema,  hivyo vilivyotolewa hospitalini hapo vitawasaidia pia wajawazito kujifungua wakiwa na uhakika na usalama wao.

"Wadau wengine wakijitokeza tutaweza kutatua changamoto hii na kuwaweka wajawazito uhakika wa usalama wao pamoja na watoto wao." Amesema.

"Sisi NSSF tunaunga mkono juhudi hizi za Serikali ya Awamu ya Tano, na leo hii Wafanyakazi Wanawake ambao tunawawakilisha Wafanyakazi wenzetu wanawake nchi mzima, tumekuja hapa katika Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala kwa ajili ya kutoa msaada wa vifaa tiba, ambao tumeutoa baada ya kujua uhitaji walionao hapa hospitali,  alisema.

Alisema vifaa tiba hivyo vina thamani ya Shilingi za Kitanzania milioni 8.7, vifaa hivyo ni pamoja na mipira kwa ajili ya kuwasaidia wanawake pale wanapojifungua au kufanyiwa upasuaji na mashuka ambavyo vifaa tiba hivyo vinahitajika sana katika Hospitali hii.

Lulu, amewashauri wanawake kutumia fao la uzazi la NSSF linalotolewa kwa wanawake pindi wanapojifungua ili waweze kulea watoto wao kwa usalama zaidi.

Kwa upande wake Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala
Dk. Nkungu Daniel , aliushukuru Mfuko wa NSSF kwa msaada wa vifaa tiba hivyo ambavyo walikuwa wanavihitaji kwa ajili ya kuwasaidia wagonjwa mbalimbali wanaopata huduma katika hospitali hiyo.

Makungu ametaka wadau wengine kufuata nyayo zinazofanywa na NSSF katika kutatua changamoto mbalimbali za kijamii ikiwemo katika sekta ya afya pia .

Naye Mwenyekiti wa Wanawake wa NSSF, Vaileth Segeja aliushukuru uongozi wa NSSF kwa kuwajali na kuwasikiliza  bila kuwabagua kama wanawake na wanafanya kazi zao kwa uhuru na wamekuwa chachu ya maendeleo.

Mmoja wa wanufaika wa msaada huo Rose Robert amewashukuru NSSF kwa kuwawekea mazingira bora zaidi katika wodi wazazi na kueleza kuwa mazingira bora huleta uhakika na usalama wa uzazi wao kabla na baada ya kujifungua.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...