RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akizungumza mara baada ya Kumuapisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo Machi 31, 2021. Hata hivyo Rais Samia amefanya uteuzi na panga pangua ya baadhi ya mawaziri katika wizara mbalimbali hapa nchini.
Kutoka Kulia ni Makamu wa Rais wa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango, Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dkt. Hussein Mwinyi, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Majaliwa Kassim Majaliwa pamoja na Makamu wa pili wa Rais wa Mapinduzi ya Zanzibar, Hemed Suleiman Abdalla wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan leo Machi, 31, 2021 mara baada ya kumwapisha Makamu wa Rais.

Baadhi ya Mawaziri na wabunge wakiwa katika Uapisho wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Munggano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango leo Machi 31, 2021.


* MWIGULU APELELWA WIZARA YA FEDHA,JAFO AONDOLEWA TAMISEMI

Na Mwandishi Wetu,Michuzi TV- Dodoma
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amefanya mabadiliko madogo kwenye Baraza la Mawaziri huku akitangaza kumteua Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Hussein Kattanga anayechukua nafasi iliyoachwa wazi baada ya Aliyekuwa katika nafasi hiyo Balozi Dkt.Bashiru Ally kumteua kuwa Mbunge.

Ametangaza mabadiliko hayo leo Ikulu ya Chamwino Mjini Dodoma baada ya kuapishwa kwa Makamu wa Rais Dkt.Philip Mpango ambapo baada ya kiapo hicho akaeleza zege halilali, hivyo amefanya mabadiliko katika baraza hilo na mawaziri wote waliofanyiwa mabadiliko wataapa kesho saa nne asubuhi.

Akitangaza mabaliko hayo, Rais Samia aliwaambia mawaziri wasiwe na wasiwasi kwani hajaacha mtu kwani ameona jinsi ambavyo sura zao zimebadilika wamejawa na hofu.

Katika baraza hilo, Waziri wa Nchi , Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa( TAMISEMI) amempeleka Ummy Mwalimu na kwa upande manaibu mawaziri hakuna mabadiloko, Wizara ya Utumishi na Utawala Bora amemteua Mohamed Mchengelwa, kwa upande wa manaibu mawaziri hakuna mabadiloko.

Rais Samia amesema kwamba aliyekuwa Waziri katika Wizara hiyo George Mkuchika atakuwa katika ofisi yake na atampangia majukumu mengine.Wizara ya Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira amemteua Seleman Jafo na Naibu wake ni Hamad Said Chande.

Wakati Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu anabaki Jenista Mhagama, Wizara wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji ni Geophrey Mwambe na Naibu Waziri William Ole Tate na ametoa miezi mitatu Wizara hiyo ianze kazi.

Wizara ya Mipango na Fedha amepelekwa Mwigulu Nchemba na Naibu Waziri Hamad Yusuf Masauni, Wizara ya Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi na Naibu Waziri Geohrey Mizengo Pinda.Katika Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa pamoja na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi hakuna mabadiliko.

Aidha Rais Samia amesema Wizara ya Ujenzi hakuna mabadiliko wakati Wizara ya Viwanda amelekwa Profesa Kitila Mkumbo na Wizara ya Madini hakuna mabadiliko.Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi hakuna mabadiliko.

Katika mabadiliko hayo Wizara ya Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo amebakia Innocent Bashungwa na Naibu Waziri amemteua Pauline Gekul.Hivyo aliyekuwa Naibu Waziri katika Wizara hiyo Abdallah Ulega amehamishiwa Wizara ya Mifugo na Uvuvi ambapo atakuwa Naibu Waziri na Waziri wake atabaki aliyepo.

Rais Samia amesema Wizara ya Elimu hakuna mabadiliko wakati Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Waziri anabaki Dkt.Doroth Gwajima, Naibu wa Waziri Dk.Mollel lakini amemuongeza Mwanaidi Ally Hamisi.

Wizara ya Nishati,Wizara ya Maliasili na Utalii pamoja na Wizara ya Mawasiliano hakuna mabadiliko. Hata hivyo Rais Samia amewataka Mawaziri na Manaibu Mawaziri kuchapa kazi na kwamba ataendelea kufuatilia utendaji wao ,wale watakaoshindwa wataishia njiani na kwamba Serikali ya Awamu ya Sita ndio imeanza kazi,hivyo kila mmoja afanye kazi.

Wakati huo huo ametangaza kuteua Wabunge watatu ambao ni Dk.Bashiru Ally Kakurwa, Mbarouk Mbarouk pamoja na Balozi Libelata Mulamula.Aidha baada ya kumteua Dkt.Bashiru kuwa Mbunge, nafasi ya Katibu Mkuu Kiongozi amepewa Balozi Hussein Katanga aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Japan.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...