1.       Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Mark Ocitti (kulia) akiongea na wanafunzi wa chuo cha Kaole Wazazi College of Agriculture cha Bagamoyo mkoani pwani ambao ni wanufaika wa program ya ufadhili wa masomo  walipotembelea kiwanda cha kampuni hiyo cha Dar es Salaam. Kushoto ni Makamu mkuu wa chuo hicho Maximillian Sarakikya


1.       Mmoja wa wanafunzi ambaye ni mnufaika wa programu ya ufadhili wa masomo unaotolewa na kampuni ya Bia ya Serengeti kutoka chuo cha Kaole Wazazi College of Agriculture cha Bagamoyo mkoani Pwani Emmanueli Ntandu, akielezea namna ambavyo programu ya ufadhili wa masomo imeweza kumsaidia kufufua ndoto yake ya kuendelea na masomo baada ya kushindwa kulipa ada na kufikia uamuzi wa kusitisha masomo yake.

1.       Meneja Afya na Usalama wa Kampuni ya Bia ya Serengeti David Mwakalobo (kulia) akifafanua jambo kwa wanafunzi wa chuo cha Kaole Wazazi College of Agriculture cha Bagamoyo mkoani pwani ambao ni wanufaika wa program ya ufadhili wa masomo unaotolewa na kampuni hiyo unayojulikana kama Kilimo Viwanda waliotembelea kiwanda cha kampuni hiyo cha Dar es Salaam.

1.       Baadhi ya wanafunzi wa chuo cha Kaole Wazazi College of Agriculture cha Bagamoyo mkoani pwani ambao ni wanufauika wa program ya ufadhili wa masomo unaotolewa na Kampuni ya Bia ya Serengeti unaojulikana kama Kilimo Viwanda, wakifuatilia mada zilizokuwa zinatolewa walipotembelea kiwanda cha kampuni hiyo cha Dar es Salaam

========  ========  ========  ==========

Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) leo imetangaza kutoa nafasi mpya 70 za ufadhili wa masomo kwa wanafunzi wanaosomea kilimo hapa nchini. Ufadhili huu unajumuisha ada pamoja na gharama nyingine zote za masomo katika kipindi chote mwanafunzi anapokuwa chuoni.

 Hii ni mara ya pili kampuni ya SBL inatoa ufadhili wa masomo kwa wanafunzi waliofanya vizuri katika masomo yao na ambao wanatoka katika familia zenye vipato duni. Mwaka jana wakati SBL ikizindua mpango wake wa ufadhili wa masomo ya kilimo unaojulikana kama Kilimo Viwanda, ilitoa ufadhili kwa wanafunzi 40.

 Programu ya Kilimo-Viwanda inalenga kuunga mkono jitihada za serikali katika kuongeza idadi ya wataalamu wa kilimo hapa nchini, kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa SBL, Mark Ocitti

 Akitangaza wanafunzi 15 waliopata ufadhili huo kwa mwaka huu kutoka chuo cha Kaole Wazazi College of Agriculture cha Bagamoyo mkoani Pwani, Ocitti alisema pamoja na kutoa ufadhili wa masomo kampuni hiyo pia inafanya kazi na wakulima 400 ambao mwaka jana waliiuzia SBL tani 17,000 za nafaka sawa na asilimia 70 ya mahitaji yake ya malighafi kwa ajili ya kutengenezea bia.

 “Uhusiano wa SBL na sekta ya kilimo una historia ndefu. Kwa sasa kampuni inafanya kazi na mtandao wa wakulima 400 kwenye mikoa nane hapa nchini ambapo tunanunua shayiri, mahindi na mtama kwa ajili ya uzalishaji wa bia zetu. SBL huwasaidia wakulima hawa kwa kuwapatia mbegu za bure, huduma za ughani pamoja na kuwaunganisha na taasisi za kifedha kwa ajili ya kupata mikopo na kupanua uzalishaji wao,” alisema.

 Mkuu wa chuo cha  Kaole Wazazi College of Agriculture, Sinani Simba, aliishukuru kampuni ya SBL kwa kuwa mstari wa mbele katika kuunga mkono maendelea ya sekta ya kilimo ambayo ni sekta mama inayoajiri Watanzania wengi kuliko sekta nyingine yeyote ile.

 “Mafunzo kwa ajili ya wataalamu wa kilimo ni moja kati ya vipaumbele kwenye Mpango wa Maendeleo ya Kilimo Awamu ya Pili. Wataalamu wa kilimo ni muhimu katika kuwasaidia wakulima kuboresha shughuli zao kwa kuwaelekeza namna ya kulima kitaalamu ili kuongeza uzalishaji na kuboresha vipato vyao,” alisema mkuu huyo wa chuo.

 Kampuni ya SBL inashirikiana na vyuo vinne vya hapa nchini katika kutoa iufadhili wa masomo chini ya Programu ya Kilimo Viwanda. Pamoja na Kaole Wazazi College of Agricultre, vyuo vingine ni pamoja na chuo cha Kilacha Agriculture Institute kilichopo Moshi mkoani Kilimanjaro, Igabiro Institute of Agriculture kilichopo Bukoba mkoani Kagera na St. Maria Goretti Agriculture Training Institute kilichopo mkoani Iringa.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...