Na Chalila Kibuda,Michuzi Tv Mtwara

Serikali imewataka watoa huduma za mawasiliano wa simu za Mkononi kufanya utafiti wa kutosha katika maeneo walioweka minara kutokana na minara iliyojengwa inaelemewa na watumiaji wa simu za Mkononi.

Hayo ameseyama Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Kundo Andrea alipofanya ziara  katika Mkoa wa Mtwara kwa kupita katika wilaya kuona changamoto za Mawasiliano.

Kundo amesema kuwa minara mingi ilijengwa miaka ya ambayo ilikuwa na wakazi wachache lakini sasa watu wameongezeka na kufanya minara hiyo kushindwa kuhudumia kwa ubora.

Aidha amesema minara hiyo katika maeneo ilijengwa kwa 2G ambapo ilikuwa kupiga simu ,kupokea pamoja na kutuma ujumbe lakini sasa wameongezeka watumiaji wa simu janja ambapo wanatakiwa kwenda katika 3G na 4G waweze kutumia kwa kupakua picha pamoja na huduma zingine.

Naibu Waziri Kundo amesema kuwa uchumi wa sasa unakwenda kwa Teknolojia ya Mawasiliano ambapo Serikali inapata mapato kutumia mifumo ambayo inahitaji kuwa Data.

Amesema muda wa kukimbizana na kalatasi unapita na kubaki na mifumo ya Teknolojia ya Habari kwendana na wakati uliopo.

Aidha amesema katika maeneo yenye changamoto ikiwemo  Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kufatilia sehemu changamoto ya kukosa ubora wa Mawasiliano.

Hata hivyo amesema sehemu zenye Umeme wanye watoa huduma za mawasiliano waunge na kuacha kutumia mafuta.

Kundo amesema katika Wilaya ya Nanyumbu,Newala,Masasi ikiwemo Mtamba wa swala mawasiliano yafike kutokana na kuwepo kwa fursa za kibiashara.

Nae Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Mhandisi Lawi Odiero amesema maagizo yote watayafanyia kazi katika kuhakikisha wananchi wanapata mawasiliano.

Mhandisi Odiero upande wa Halmashauri zinazo  hitaji leseni za uanzishaji Radio atahakikisha wanawasiliana katika kufuata utaratibu wa maombi ya radio.

Waziri wa Nishati Dkt.Medard Kalemani akímueleza Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Kundo Andrea walipokutana ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara kuhusiana upatikanaji wa. Umeme katika minara ya simu za Mkononi ikiwa kila mmoja ana ziara katika Mkoa huo.
Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Kundo Andrea akizungumza katika Ofisi ya Mkoa wa Mtwara kuhusiana na mawasiliano walivyojiwekea kuhakikisha wananchi wanapata mawasiliano yaliyo bora.
Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa TCRA Mhandisi Lawi Odiero akitoa ufafanuzi kwa Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Kundo Andrea katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mtwara.
Katibu wa Chama cha Mapunduzi (CCM) akizungumza katika ziara ya Naibu Waziri Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi  Kundo Andrea alipotembelea Ofisi hiyo.
Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Kundo Andrea akizungumza katika Ofisi za CCM Mkoa wa Mtwara alipofanya ziara na kueleza sehemu ya Ilani kuhusiana na Sekta ya Mawasiliano.
Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Kundo Andrea akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa TTCL Mkoa wa Mtwara Fredrick Mloka wakati alipofanya ziara hapo.
Meneja wa Shirika la posta Mkoa wa Mtwara akitoa maelezo ya Shirika kwa Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Kundo Andrea alipofanya ziara hapo
Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Kundo Andrea akipata maelezo kutoka kwa mwananchi wa kijiji cha matembezi wilayani Nanyumbu alipofanya ziara ya kuangalia hali ya Mawasiliano katika kijiji hicho.
Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Kundo Andrea akitimisha ziara ya Mkoa wa Mtwara katika daraja la mtambawaswala lilopo mpakani mwa Tanzania na Msumbiji majira ya saa moja usiku.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...