Na Woinde Shizza , Michuzi Tv-ARUSHA

Asasi ya kilele inayojishughulisha na kilimo horticulture yaani mboga, matunda, mimea itokanayo na mizizi, pamoja na viungo (TAHA) imejipanga kuwawezesha wanawake kuzalisha mazao kutokana na mahitaji ya soko, ili kupata mavuno bora na yenye uwezo wa ushindani katika soko la ndani na nje ya nchi.

Hayo yamebainishwa na meneja biashara mwezeshaji Kelvin Remen wakati akiongea na waandishi wa habari kuhusiana na namna asasi yao ilivyoweza kuwasaidia wanawake kuelekea maathimisho ya siku ya wanawake dunia ya mwaka 2021 ambavyo kauli mbiu yake inasema "wanawake katika uongozi chachu kufikia dunia yenye usawa " ambapo alisema kupitia kauli mbiu ya TAHA “Horticulture for Health and Wealth”, wana dhamira ya kubadilisha Maisha ya wanawake kwa kuwahamasisha wajikite katika kilimo cha mazao ya horticulture ili kuongeza kipato na kuboresha lishe kupitia kilimo hicho.

Alisema wamejipanga kuwawezesha kirahisi katika upatikanaji wa masoko ya bidhaa za Horticulture, kupata nyenzo muhimu na rasilimali za uzalishaji,Kuwafikishia huduma za kitaalamu na ushauri kwa makundi ya mnyororo wa thamani ,kuboresha ushiriki wa wanawake katika michakato ya kufanya maamuzi katika minyororo ya thamani pamoja na Kuongeza upatikanaji fursa za uwekezaji kwa wanawake kwenye minyororo mzima wa thamani.

Aidha alisema kuwa hapo awali, kulikuwa na mzigo mzito wa wanawake wa majukumu ya kaya hivyo kupunguza wakati na nguvu zao kwenye fursa za kilimo na kilimo, kama vile kupata ujuzi na taarifa.

"Kwa mfano, kulingana na utafiti uliofanyika na uwanja wa taasisi ya Bill&Melinda Gates , uliofanyika mwaka 2014 wanawake wazalishaji wadogo hufanya kazi kwa takriban masaa 14 kwa siku, ambayo masaa 8-9 walijitolea kwa shughuli zisizo za kuingiza kipato kulipwa za kilimo ,"

Alisema katika kumsaidia mwanamke TAHA imeanzisha mashamba ya mfano (Demonstation plots) zaidi ya 1000 na vituo vya mafunzo kwa vitendo saba ambavyo vipo wazi wakati wote,hii imetoa fursa kwa wanawake wengi kupata mafunzo kupitia vituo hivyo na kuongeza ushiriki wao katika shughuli za kilimo .

Alibainisha ukilinganisha na miaka ya nyuma, asilimia ya wanawake ambao wamejiajiri kwenye kilimo cha Horticulture imeongezeka kutoka asilimia nane mpaka asilimia 65 kwenye maeneo ambapo TAHA inafanya shughuli zake , hii inamaanisha kwamba kati ya wakulima walioko kwenye mnyororo wa thamani ambapo asasi yao inafanya miradi yake takribani asilimia 60 na wanawake.

Alisema kulingana na tamaduni, wanawake kujihusisha kutafuta masoko huwa ngumu hasa masoko ya mbali, kulingana na umbali wa mashamba yalipo, safari ya kwenda sokoni inaweza kuchukua siku tatu, Mazingira ya soko yanayotawaliwa na wanaume yanaweza kuwa yasiyo rafiki na salama kwa wanawake ambao lazima walale, au kwenda sokoni kabla ya mapumziko ya siku.

Alisema taasisi ya bill&melinda Gates Foundation (BMGF)2014 inawapa wanawake mamlaka ndogo ya kufanya maamuzi kuhusu lini, wapi na kwa kiasi gani cha kuuza mazao yao yanayotakiwa kulimwa kwa msimu huo ,Kutokana na elimu zinazotolewa mara kwa mara za kujenga uelewa kwa jamii juu ya ushiriki wa mwanamke katika shughuli za maendeleo mambo yamebadilika. pamoja na mengineyo, ambapo TAHA ina mfumo wa taarifa wa masoko (Marketing Information System) yenye wasajiliwa zaidi ya 41,000 (wakulima na wafanyabiashara) ambapo zaidi ya asilimia 30 ni wanawake. Kupitia mfumo huu wanawake wanaweza kupokea taarifa mbalimbali za masoko ya bidhaa za horticulture kama vile bei, wanunuzi, usafirishaji kupitia simu zao za mikononi, mahali popote walipo

Alisema wanaweza kuona uwiano wa wanawake ambao wanajiingiza kwenye masoko makubwa umeongezeka, hapo nyuma kati ya wadau wao wanaojiingiza kwenye masoko hayo wanawake hawakufika hata asilimia 15%, Ila kwa Sasa wameanza kuona ongezeko kubwa la wanawake wanaojiingiza kwenye masoko makubwa ya kikanda na kimataifa ambapo ni zaidi ya asilimia 30 ,hii ni mara mbili ukilinganisha na hapo awali, wanatumaini jinsi wanavyoendelea kuelimisha jamii, ushiriki wa mwanamke utaongezeka mara dufu katika kipindi cha miaka michache ijayo.

Kwa upande wake Mkulima wa zao la papai Epiphania Buhogwa alisema kuwa Taha wameweza kumsaidia kwa kiasi kikubwa Sana kwani awali alikuwa akilima lakini hapati mahali pa kuuzia ,masoko yalikuwa hamna na awapo alikuwa akiyapata alikuwa akiuza kwa bei ya chini Sana lakini tangu ajiunge nao amekuwa akilima kwanza kilimo Cha kisasa ambacho pia kimasaidia kupata mazao mengi .

Alisema pia baada ya kulima papai kwa muda mrefu alipatiwa ushauri pia na taha kulima zao la pasheni na kuelekea kuwa zao hilo lina masoko sana na alipo lima ilimsaidia kwani anaweza kuvuna na kujiongezea kipato ,kulipia watoto ada pamoja na kuendesha maisha yake.

Aliwataka wanawake kuamka na kuacha kuwa tegemeze badala yake wajishughulishe Ili waweze kusaidia familia zao Katika majukumu mbalimbali.

 Mkulima Joyce Samweli akiandaa mazao kwajili ya kuotesha mwanamke huyu ameweza kujenga nyumba ya nne pamoja na kununua mifugo kwa fedha zilizotokana na kilimo(picha na Woinde Shizza, ARUSHA).

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...