Brigedia Generali John Julius Mbungo  Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (TAKUKURU) , Taasisi inayosimamia haki za wananchi hapa nchini.

Msimamizi wa mirathi wa familia ya Ally Segamba ya Kijiji cha Ujamaa Palaka kilichopo wilayani Kisarawe, ambaye ni mfuatiliaji wa malipo hayo. 



Na Mwandishi Wetu


WAKALA wa Barabara Tanzania, (TANROAD) Mkoa wa Pwani unatarajia kuilipa sh.milioni 6  familia ya Ally Segamba ya Kijiji cha Ujamaa Palaka kilichopo wilayani Kisarawe.

Fedha hizo ambazo kwa mujibu wa familia hiyo ni Shilingi Milioni 6,60,000 ni kwa ajili ya malipo yaliyotokana na Tanroad kuingia mkataba na familia hiyo Desemba 10, mwaka jana kuchimba kokoto kwenye shamba lao.

Akizungumza na waandishi wa habari hivi karibuni Segamba alisema tangu mkataba huo kwisha walifuatilia malipo yao Tanroad bila mafanikio baada ya kuwekewa  mizengwe ya hapa na pale.

“Tulipoona tunafuatilia tulipwe fedha zetu bila mafanikio tuliandika barua ya malalamiko kwa uongozi wa Tanroad ambayo nakala tulizipeleka kwa Rais John  Magufuli, Mkurugenzi wa Takukuru nchini, Takukuru Mkoa wa Pwani na kwa Maveretani wa UVCCM Taifa kuomba msaada wao,” alisema mwanafamilia huyo.

Aliongeza walifikia hatua hiyo baada ya kuona Tanroad wamekiuka makubaliano yaliyomo kwenye mkataba yanayoelekeza malipo yao yafanyike siku saba baada ya mkataba kwisha lakini wao hawajafanya hivyo.

“Tulichobaini kinachowafanya Tanroad watusumbue kutulipa kuna baadhi ya watendaji wa wakala hao wa barabara mkoa wa Pwani kutaka wapewe mgawo kwa kisingizio cha mtu ambaye hahusiki katika shamba letu waliyemtengenezea nyaraka feki ili naye aonekane ni mmiliki wa shamba letu waliyeingia naye mkataba wa kuchimba kokoto katika shamba letu la mirathi ili fedha hizo zitakapolipwa naye apewe mgawo ambao watagawana.”

Gazeti hili lilipo wasilia na Mhandisi wa Tanroad mkoani humo,  Livingstone Urio aliyekuwa miongoni mwa maafisa wa Tanroad waliosaini mkataka huo, alikataa kuzungumza chochote kwa kuwa si msemaji ambapo alimtaka mwandishi wetu awasiliane na Meneja wa Tanrod wa mkoa,  Mhandisi  Yudas Msangi.

Msangi alikiri kuufahamu mkataba huo na kuahidi kuilipa familia hiyo fedha zao ndani ya wiki mbili baada ya mkandarasi kuandaa malipo yao na kuwapelekea.

“Siyo kwamba hatuwalipi, tulikuwa tunasubiri mkandarasi anayesimamia miradi mingi aandae malipo yao atuletee ndipo tuwalipe, jana (juzi) ndiyo katuletea hivyo tutawalipa ndani ya hizi wiki mbili, lakini wao wenyewe wanamigogoro hivyo pesa hizo tutazipeleka kule kijijini,” alisema Msangi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...