Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo akichana mfuko uliowekewa mche wa mti kabla ya kuupanda , leo Machi 6,2021 katika eneo la nje ya geti la Hifadhi ya Msitu Asilia wa Pugu Kazimzumbwi uliopo wilayani Kisarawe mkoani Pwani.Wadau wa uhifadhi na mazingira kutoka maeneo mbalimbali nao wameshiriki kwenye shughuli ya upandaji miti katika eneo hilo ikiwa ni sehemu ya matukio yaliyopo kwenye tamasha la Kisarawe Ushoroba Festival.
Jokate Mwegelo ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani, akifukia udongo baada ya kupanda mti katika eneo la Hifadhi ya Msitu Asilia Pugu Kazimzumbwi leo ambapo wadau wengine mbalimbali nao wameshiriki upandaji miti.
Katibu Tawala Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani Mwanana Msumi akizungumza katika siku ya pili ya tamasha la Kisarawe Ushoroba Festival kabla ya Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo kuzungumza na wananchi wa wilaya hiyo pamoja na wadau mbalimbali walihudhuria tamasha hilo.
Baadhi ya wadau wa mazingira wakipanda miti.
Mwakilishi kutoka Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS) Bakari Mohamed akizungumza kwenye tamasha hilo alipokuwa akimwakilisha Kamishna wa Uhifadhi Profesa Dos Santos Silayo.
Muonekano wa Hifadhi ya Msitu Asilia wa Pugu Kazimzumbwi unavyoonekana
Maofisa wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS) wakiongozwa na Kaimu Meneja Mawasiliano wa Wakala huo Martha Chassama (wa pili kulia) wakiwa katika picha ya pamoja nje ya banda la Wizara ya Maliasili na Utalii lililopo kwenye tamasha la Kisarawe Ushoroba Festival.

Na Said Mwishehe, Michuzi TV

WAKALA wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS) umetoa mwito kwa wananchi, wadau na wakawekezaji wa ndani na nje ya nchi kwenda kuwekeza katika misitu ya Serikali ambayo inahifadhiwa na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania ukiwemo Msitu wa Hifadhi ya Mazingira Asilia Pugu Kazimzumbwi ulioko wilayani Kisarawe mkoani Pwani.

Aidha Wakala huo umesema katika kuhakikisha uhifadhi wa mazingira pamoja na utalii ikolojia unakuwa endelevu, wamekuwa na utaratibu wa kuwa na programu za kutoa elimu kwa watoto ili kutambua mapema kuhusu uhifadhi wa misitu na faida zake, pamoja na kuwahamasisha kupanda miti.

Akizumza leo Machi 6, mwaka 2021 baada ya tukio la upandaji miti lililoongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo lililofanyika katika Msitu wa Pugu Kazimzumbwi ikiwa ni sehemu ya shughuli zilipo katika Tamasha la Kisarawe Ushoroba Festival Kaimu Meneja Mawasiliano TFS Martha Chassama amesema ni jukumu la kila mmoja wetu kuhakikisha anakuwa mdau katika eneo la uhifadhi wa mazingira na kuhamasisha utalii hasa wa kutemmbelea hifadhi za misitu ya asili.

Kuhusu TFS kuendelea kutoa elimu kwa umma kuhusu umuhimu wa uhifadhi wa misitu nchini, amesema mbali ya kutoa elimu kwa wadau mbalimbali wamekuwa wakitoa elimu kwa watoto kwa kutambua watoto ndio wahifadhi wa kesho, watoto ndio watalii wa kesho.

"Kwa msingi huo ndio maana leo kwenye tukio la upandaji miti watoto nao wameshiriki kikamilifu, wamepanda miti, lakini watoto wameedelea kupewa elimu ya uhifadhi, hivyo sisi TFS kutoa elimu ka watoto wadogo ni jambo muhimu na tunalipa kipaumbele.

"Tunataka mtoto akiendelea kukua anajua umuhimu wa kutunza mazingira, kutunza misitu ya asili, kutunza uhifadhi lakini mtoto awe anapenda kupanda miti ya matunda, asili, miti ya kivuli pamoja na miti yakiimani,"amesisitiza Chassama.

Kuhusu tamasha la Kisarawe Ushoroba Festival, amesema ni tamasha ambalo limesaidia kuendelea kuelezea hifadhi ya msitu wa asili ya Pugu Kazimzumbwi ambao uko chini ya TFS.

"TFS tumetengeza umakini kwa watu wanaoishi maeneo ya msitu Kazimzumbwi, katika masuala ya uhifadhi wananchi wameendelea kuwa na uelewa na tumehamasisha upandaji miti,"amesema na kusisitiza katika msitu huo TFS wanahamasisha wadau kuwekeza kwani kwa mujibu  wa sheria wanalo jukumu la wao kuuendeleza.

Akizungumzia msitu huo wa Pugu Kazimzumbwi, amesema pamoja na aina nyingine ya utalii, kuna utalii ikolojia ambao ni utalii tulivu na watu wanaweza kwenda katika utalii huo.

"Utalii ikolojia ni utalii ambao unaambatana na utulivu, sio utalii wa kuona wanyama, ni utalii ambao mtu anaweza kufanya tahajudi kwa maana ya kufanya maombi kwa muumba wake.Aidha katika msitu wa utalii ikolojia mtu anaweza kupeleka mgonjwa kwa ajili ya kufanya mazoezi katika eneo ambalo limetulia na halina vurugu,"amesema.

"Sehemu kama hizi unaweza kumleta mgonjwa ukamtembeza umbali wa kilometa moja, mbili au tatu na hasa kwa wagonjwa waliofanyiwa operesheni,"amesisitiza Chassama huku akiendelea kuhamasiaha wananchi kujenga utamaduni wa kutemebelea msitu huo.

Awali Kamishna wa Uhifadhi Prof. Dos Santos Silayo amefafanua katika misitu huo wa Pugu kuna aina mbalimbali za vivutio vya utalii na vingine hakuna mahali vinakopatikana zaidi ya ndani ya msitu huo tu.

"Kuna miti ya aina mbalimbali, kuna mazingira mazuri lakini pia kuna ndege wadogo ambao wako hapa tu.Aidha kuna ndani ya msitu huu kuna mito yenye chemchem za maji, kwa hiyo tamasha hili la Kisarawe Ushoroba Festival limekuja wakati muafaka na lina faida nyingi.

"Kwa hiyo tamasha hili tumeona tunayo sababu ya kuungana na Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe kuhakikisha tunashirikiana naye katika kila hatua, na tunamani kuona likiendelea kuwa endelevu kwa kufanyika kila mwaka,"amesema.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...