Mhifadhi Misitu Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani Fredy Ndandika akielezea umuhimu wananchi kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo wilayani Kisarawe mkoani Pwani wakati wa tamasha la Kisarawe Ushoroba Festival likiendelea kuenzia leo Machi 5 hadi Machi 7 mwaka huu.Tamasha hilo limezinduliwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo.
Mhifadhi Misitu Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani Fredy Ndandika akisisitiza jambo wakati wa tamasha la Kisarawe Ushoroba Festival linaloendelea wilayani humo.
 wa Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani Jokate Mwegelo akizungumza mbele ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais ,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo wakati wa uzinduzi wa Kisarawe Ushoroba Festival.Pia kulikuwa na wageni wengine wa kada mbalimbali pamoja na wananchi.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI)Seleman Jafo akizungumza wakati wa akizindua tamasha la Kisarawe Ushoroba Festival leo Machi 5 mwaka 2021 wilayani Kisarawe mkoani Pwani.Lengo la tamasha hilo ni kutangaza vivutio vya utalii pamoja na uwekezaji wilayani humo.
 
Na Said Mwishehe, Michuzi TV

WAKALA wa Misitu  Tanzania (TFS), umewaomba wananchi hasa wakazi wa mkoa wa  Dar es Salaam, Pwani, Morogoro na mikoa mingine  ya jirani, kutembelea vivutio vya utalii vilivyoko wilayani Kisarawe mkoani Pwani ukiwamo msitu wa Kazimzumbwi ambao ndani yake kuna vivutio vya kipekee.

Akizungumza katika banda la Wakala huo ambao lipo kwenye tamasha la Kisarawe Ushoroba Festival wilayani Kisarawe mkoani Pwani leo, Mhifadhi Misitu Wilaya ya Kisarawe, Fredy Ndandika amesema moja ya maeneo yanayostahili kutembelewa na wanachi na  wakafurahia ni Msitu wa Kazimzumbwi uliopo wilayani humo.

Amefafanua kwamba msitu huo wa asili wa Kazimzumbwi unapatikana wilayani Kisarawe na una vivutio vingi ikiwamo hali ya utulivu ambayo humpendeza kila mmoja anayeutembelea."Ndani ya msitu huo kuna njia za watembea kwa miguu na mapango ya popo, mapango ya mizimu ambayo jamii ya wazaramo huyatumia kwa ajili ya matambiko na kuomba.

 "Kivutio kingine knachopatikana katka wilaya ya kisarawe na ambacho anashauri wananchi wajitokeze kutemblea ni bwawa la Minaki ambalo hutumika kwa ajili ya utalii wa uvuvi na kupiga picha,"amesema Ndandika.

Aidha amesema vivutio vingine ni maeneo ya kupumzikia yenye sifa ya kuwa na hewa safi huku pia kukiwa na maeneo ambayo yatamwezesha mtu kusimama na kuona kwa uzuri mandhari ya mji wa Dar es saalam.

Ameongeza msitu wa Kazimzumbwi ndio pekee unaotegemewa kwa kunyonya hewa chafu izalishwayo Dar es Salaam na maeneo yaliyo jirani na Kisarawe.

"Tupo kwenye tamasha la utalii la Kisarawe Ushoroba Festival ambapo lengo kuu la tamasha hili ni kutangaza utalii na vivutio vya utalii vilivyopo ndani ya wilaya ya Kisarawe na kuonyesha fursa za uwekezaji katika wilaya yetu.

"Katika wilaya ya Kisarawe kuna maeneo mawili ya kiutalii; utalii wa kiutamaduni na utalii wa kiikolojia. Huu utalii wa Ikolojia unapatikana katika Hifadhi ya Mwalimu Nyerere ambayo sifa yakeya pekee ni kuwa hifadhi kubwa zaidi nchini," amesema.

Ameongeza TFS ndiyo iliyopewa jukumu la kusimamia hifadhi ya Mwalimu Nyerere na kwamba watatumia vyema siku tatu za taasha Kisarawe Ushoroba Festival kutangaza fursa zilizopo ili kuvutiwa watalii na wawekezaji.

Awali akizungumza katika ufunguzi wa tamasha hilo, Mkuu wa Walaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo amesema wameamua kuchochea juhudu za kutangaza utalii wilayani mwake ili kutengeneza fursa za ajira na kuwwezesha wananchi wengi kuona vivutio mbalimbali viliyoko Kisarawe.

"Nawapongeza TFS kwani tumekuwa tukishirikiana kwa karibu tangu mwanzo wa majadiliano kuhusu kufanikisha tamasha hili, hivyo nawatambua kama ni wadau wakubwa wakiwamo wadau wengine mbalimbali,"amesema.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...