KAMPUNI ya mafuta ya Total Tanzania, imekabidhi zawadi kwa washindi waliofanikiwa kubashiri timu mbili zilizoingia kwenye nusu fainali ya Total Chan 2020 michuano iliyofanyika nchini Cameroon kuanzia Januari 16 na kufikia tamati mnamo Februari 7 mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kukabidhi zawadi hizo  Mkurugenzi wa uhusiano wa makampuni kutoka Total Marsha Msuya Kilewo amesema kuwa, Total ambao ni wadhamini wakuu wa mashindano ya CHAN, CAF na AFCON  wamekuwa wakiendesha kampeni mbalimbali za kurudisha tabasamu na shukrani kwa jamii na katika shindano hilo zaidi ya washiriki 200 walijitokeza na kushiriki.

''Mashindano ya CHAN 2020, iliwapatia wateja wetu fursa ya kushindania Tv 5 aina ya Samsung HD yenye nchi 40 na ili kushinda ilihitajika mtu kubashiri timu mbili zitakazoingia fainali na ubashiri huu ulikuwa ni wa kidigitali na washindi walioibuka kidedea ni pamoja na Amani Ephraim, Innocent Mchimo, Salehe Athumani, Godbless Mboya naStephen Emanuel. Tunawashukuru sana kwa ushiriki na hongereni kwa ushindi wenu.'' Amesema.

Amesema Televisheni hizo zina thamani yazaidi ya shilingi laki saba  kila moja na  ameishukuru Bodi ya michezo ya kubahatisha (Gaming board,) kwa kusimamia vyema michezo hiyo inayowawezesha watanzania  kushiriki na kujishindia zawadi kambambe.

Pia amewataka watanzania kuendelea kutembelea vituo vya mafuta vya Total kote nchini ambako watapata huduma huduma zote kwa viwango vya juu kabisa ikiwemo mafuta yenye viambata vinavyosafisha engine kilomita kwa kilomita, huduma za kuosha magari, kubadilisha mafuta na kununua bidhaa za nyumbani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...