VIONGOZI wa kidini na
wale wa vyama vya siasa Zanzibar wamesema kuwa malim Seif sharif Hamad ni mtu
aliyemaliza muda wake wa kuishi katika ulimwengu akiwa amewacha mafanikio makubwa.
Hayo wameyasema katika kanisa la PEFA church of Zanzibar nje kidogo ya mji wa Zanzibar huko Kisauni wakati wakitoa historia ya marehemu maalim Seif Sharif Hamad katika hafla ya kumbukumbu ya kusherekea maisha ya kiongozi huyo aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha ACT wazalendo.
Viongozi hao wamelezea kuwa
wanakila aina ya sababu ya kumkumbuka na kumuenzi kiongozi huyo kutokana na kile
walichokisema wema mkubwa aliowatendea wazanzibar.
“Maalim alikuwa kiongozi wa aina ya kipekee na mwenye kuipenda Zanzibar na watu kutoka ndani ya moyo wake kwa nini tusimkumbuke.” walisema viongozi hao.
Naibu Katibu mwenezi wa
chama cha mapinduzi (CCM) Zanzibar Katherin
Pitanao alisema kuwa kiongozi huyo amemaliza muda wake akiwa
na kila alama ya wema.
Alisema Malim seif amekwenda kwa baba akiwa ameiacha Zanzibar salama na wala hawana mashaka na mtu aliyetangazwa kushika nafasi ya malim Seif wana imani Zanzibar itatengamaa.
Katherina ameleza ana imani kuona Zanzibar inakwenda mbele zaidi na hana mashaka na Dk husein Mwinyi kwani ameonesha wazi kutaka umoja , maendeleo na kuinua uchumi imara wa Zanzibar.
Alisema hana mashaka na viongozi waliopo sasa anajua wanayo dhamira ya kweli ya kuitumika nchi hii sambamba na kuendelea kuwa na mshikamano wa pamoja.
“Sisi tuliamini maalim Seif ameacha mali kwa muda aliotumikia nchi hii tuliamini ameacha majumba Dubai ana majumba Dar es Salaam ana majumba Zanzibar lakini hapana amekwenda akiwa maskini amekwenda kama alivyokuja hakuacha mali yeyote”Alisema Katherina .
Muwakilishi kutoka katika
dini ya kikristo Joshua Goma amesema malim amekuwa mfano mzuri kwa
kuwaunganisha na kuwaeka pamoja watu
ambao walikuwa wametofautiana kutokana na vyama vyao .
Amesema ni wajibu wa vyama vya siasa kuchukua nafasi ya kunganisha watu bila ya kujali itikadi zao za kisiasa kwani kufanya hivyo ni kuwa na uono wa mbali .
Naibu Katibu mkuu wa
Chama Cha ACT Wazalendo Nassor Ahmed Mazrui
amesema Marehemu maalim Seif Sharif Hamad
ameacha urathi ambao unataka kuendelezwa
ili Zanzibar ifike pale inapotaka kwenye uchumi wa bluu.
Mazrui amesema bila ya
kuendelezwa yale aliyoyacha umoja maelewano na mshikamano Zanzibar haiwezi kufika pale inapotakiwa
kufika.
Kwa upande wake afisa kutoka ofisi ya Makamo wa kwanza wa rais
Makame Khatib Makame amezitaka tasisi zote nchini kuiga wigo wa kumkumbuka Maalim
Seif kwa kwa kuyaenzi yale mazuri aliyoyawacha.
“Tumkumbuke Maalim Seif
kwa azma yake ya kuleta umoja na mshikamano nchini Sote tusimame kwa msingi wa
kuepuka rushwa na ubadhirifu na kuweka upendo miongoni mwetu.”alisema Makame.
Amesema kuwepo kwake kumeleta
mashirikiano ya msingi wa kuwaleta watu pamoja na Zanzibar imepata mafanikio ya
kutosha.
“Tunamkumbuka Maalim Seif kwa kutuachia ushirikiano
hatuna budi kila mmoja kuendeleza kwa nguvu zote”alisema Makame.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...