Waziri wa TAMISEMI, Mhe. Suleiman Jafo  (kushoto ),  Naibu waziri Habari,  Utamaduni, Sanaa na Michezo,  Mhe. Abdallah Ulega (ambaye alikuwa mgeni rasmi ), Meneja wa Vodacom Tanzania Foundation, Sandra Oswald, na Mhifadhi Mazingira kutoka WWF, Dkt. Severin Kalonga wakiwa kwenye picha ya pamoja na washindi wa jumla wa kilomita  21 mbio za Kisarawe Ushoroba Marathon 2021 Omary Maulidi (katikati ) , Rebecca Machege  (kushoto ) na Grace Charles.  Mbio hizo zilifanyika wilayani Kisarawe jana. Vodacom ilidhamini mbio hizo zenye lengo la kudhibiti mabadiliko ya tabia nchi kupitia upandaji miti na utunzaji wa mazingira.

Waziri wa TAMISEMI, Mhe. Suleiman Jafo,  Naibu Waziri Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Abdallah Ulega, Mkuu wa wilaya ya Kisarawe, Mhe. Jokate Mwegelo na Meneja wa Vodacom Tanzania Foundation, Sandra Oswald wakishikilia utepe kabla ya kuanza kwa mbio za kilomita 21 za Kisarawe Ushoroba Marathon 2021 zilizofanyika wilayani Kisarawe. 
Waziri wa TAMISEMI, Mhe. Suleiman Jafo akibadilishana mawazo na Meneja wa Vodacom Tanzania Foundation, Sandra Oswald na Mhifadhi Mazingira WWF, Severin Kalonga. 
Mshindi wa mbio za Kisarawe Ushoroba Marathon 2021 kwa kilomita 21 wanaume, Omary Maulidi wa Dar es Salaam akimaliza mbio hizo kwa kutumia muda wa saa 1:12.
Washindi wa kilomita 10 mbio za Kisarawe Ushoroba Marathon wakiwa kwenye picha ya pamoja na Waziri wa TAMISEMI, Mhe. Suleiman Jafo, Meneja wa Vodacom Tanzania Foundation, Sandra Oswald na Mhifadhi Mazingira WWF, Severin Kalonga 

Mkuu wa wilaya ya Kisarawe, Mhe. Jokate Mwegelo akimvisha medali mshindi wa kwanza wanawake kilomita 5,  Assumpta Lameck. 

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...