Mtaalam wa maabara wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Jesca Mlay akimtoa damu mchezaji wa timu ya taifa chini ya miaka 17 Serengeti Boys Abdul Libandika kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa magonjwa ya moyo wakati wachezaji 24 wa timu hiyo walipofika katika taasisi hiyo kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa magonjwa ya moyo kabla ya kushiriki mashindano ya kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) yatakayofanyika nchini Morocco katikati ya mwezi huu.
Mtaalam kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Nuru Lugawa akimpima uzito na urefu mchezaji wa timu ya taifa chini ya miaka 17 Serengeti Boys Mohamed Mbarak wakati wachezaji wa timu hiyo walivyofika JKCI kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa afya ya moyo kabla ya kushiriki mashindano ya kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) yatakayofanyika nchini Morocco katikati ya mwezi mwezi huu.
Baadhi ya wachezaji wa timu ya taifa chini ya miaka 17 Serengeti Boys wakisubiri kufanyiwa uchunguzi wa magonjwa ya moyo leo katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI). Wachezaji 24 wa timu hiyo walifanyiwa vipimo vya kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi, umeme wa moyo unavyofanya kazi na damu ikiwa ni mojawapo ya kutekeleza sheria ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) kwa kila mchezaji anayeshiriki mashindano hayo kupima. Picha na: JKCI

Fundi sanifu wa moyo (Cardiovascular technologist) wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Jasmin Keria akimpima mfumo wa umeme wa moyo unavyofanya kazi (Electrocardiography – ECG) kapteni wa timu ya taifa chini ya miaka 17  Serengeti Boys Ladaki Chasambi wakati timu hiyo ilipofika JKCI kwa ajili ya kuwafanyiwa uchunguzi wa magonjwa ya  moyo kabla ya kushiriki mashindano ya kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) yatakayofanyika nchini Morocco katikati ya mwezi huu.
Afisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Gudila Swai akimpima shinikizo la damu mchezaji wa timu ya taifa chini ya miaka 17 Serengeti Boys Silverster Otto wakati wachezaji wa timu hiyo walipofika JKCI kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa magonjwa ya moyo kabla ya kushiriki mashindano ya kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) yatakayofanyika nchini Morocco katikati ya mwezi huu.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...