WAFANYABIASHARA, mafundi wa umeme pamoja na wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam wamelitaka Shirika la viwango Tanzania(TBS) kutoa ufafanuzi wa nyaya  zinazopaswa kuwepo katika soko ili kuwaondolea mkanganyiko wa matumizi wa nyaya hizo.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti na waandishi wa habari, wafanyabiashara pamoja na wananchi hao wamesema, kwa namna hali ilivyo sasa ni ngumu kwao wao kutambua nyaya zipi hususani za uunganishaji wa umeme majumbani zinapaswa kuwepo madukani na nyaya zipi hazitakiwi kuwepo.

Kwa mujibu wa wananchi hao akiwemo Fikiri Shaaban amesema, hapo awali TBS ilitangaza kusitishwa kwa matumizi ya nyaya nyekundu na nyeusi na badala yake zitumike rangi ya blue, kijani na rangi ya ugolo 'brown' kulingana na mahitaji ya soko la kimataifa.

Amesema kufuatia agizo hilo, baadhi yao waliamua kuachana na matumizi ya nyaya hizo zilizozuiliwa na kununua nyaya zenye rangi iliyopendekezwa ili kuepuka kuvunja sheria  ambayo kimsingi ilitaka agizo hilo kutekelezwa.

Kwa upande wake Mathias Mtinangi anayefanya shughuli zake eneo la Karikoo amesema  licha ya agizo hilo kutolewa, bado nyaya hizo zenye mchanganyiko wa rangi nyeusi na nyekundu zimeendelea kuuzwa katika maduka mbalimbali jambo aliloomba lifuatiliwe.

"Hii inatuchanganya sana sisi watumiaji na wafanyabiashara kwa kuwa tunajua kuendelea kutumia nyaya hizo ni sawa na kuvunja utaratibu,  tunaomba suala hilo lifuatiliwe ikibidi  kufanya ukaguzi katika viwanda vyote vinavyozalisha ili wahusika wabainike." amesema Mtinangi.

Bila kuvitaja viwanda hivyo, amesema ni wazi kuwa vinakiuka kwa makusudi agizo hilo la TBS ambayo kimsingi ndiyo chombo cha Serikali kilichopewa dhamana ya kusimamia viwango vya bidhaa mbalimbali zinazozalishwa ama kuingizwa nchini.

Aidha kwa uchunguzi wao wamebaini pia zipo baadhi ya nyaya hizo ambazo zimezuiliwa matumizi huingizwa hapa nchini na moja ya kampuni hivyo kutaka uchunguzi zaidi kufanyika.

Wamesema kwa sasa nyanya hizo bado zinaendelea kuuzwa katika baadhi ya maduka hususani yaliyopo mitaa ya Narung'ombe na Gogo yaliyopo Kariakoo Jijini Ilala mkoani Dar es Salaam.

Kushoto ni mfano wa nyaya zilizoagizwa kufanyiwa mabadiliko ili kufanana na nyaya za kulia.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...