Wafanyabiashara wa Soko Kuu Jijini Arusha pamoja na wanachi wenye makazi ya jirani na soko hilo wamempongeza Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini Mrisho Mashaka Gambo kwa kutimiza ahadi yake ya kuwachimbia kisima cha maji Safi na salama.

Akizungumza kwa niaba ya wafanyabiashara wa Soko KUU Jijini Arusha  Bi. Mwantum Shabani ameeleza "Tunamshuru mbunge wetu kwa kweli ametufurahisha kwa kutimiza ahadi yake ya mradi huu wa maji aliotuahidi kipindi cha kampeni zake , kwa kweli tumeteseka sana kwa muda mrefu bila maji hapa sokoni ila kwa sasa kero yetu imepata utatuzi"

Kwa Upande wake Diwani wa Kata hiyo Mhe.Tojo amempongeza Mbunge Gambo na kusema kuwa "Kata ya kati leo hii imeandika historia mpya na nikipongeze *Chama cha mapinduzi kwa kumuamini Gambo hatimaye leo hii tumepata maji safi.

Mbunge wa Arusha Mjini pamoja na kupigwa vita kwenye utendaji kazi wake lakini ameendelea kuwa ni tumaini la wananchi wa Jimbo la Arusha Mjini.

Wananchi wa Jimbo la Arusha Mjini wameonyesha kufurahishwa na style hii ya Gambo ya kujielekeza kwenye vitendo zaidi ikiwa ni pamoja na kuwa sauti ya Wananchi wa Jiji la Arusha.

Gambo kabla ya kuchimba Kisima cha Soko KUU alianza kwa kuchimba kisima cha Soko la Kilombero Jijini Arusha.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...