Na Zainab Nyamka, Michuzi Tv
Katika
kuadhimisha siku ya wanawake duniani 2021 yenye kauli mbiu ya usawa kwa
wote, Shirika la Posta Nchini limesema wanawake ni chachu ya maendeleo
na ongezeko la pato ndani ya taasisi hiyo.
Aidha,
Shirika la Posta limesema litaendelea kutoa kipaumbele kwenye nafasi
kubwa ya uongozi kwa wanawake katika taasisi hiyo pale inapohitajika.
Maadhimisho
ya siku wanawake duniani yanafanyika kila ifikapo Machi 08, ya kila
mwaka na kwa mwaka huu yaliweza kuambatana na maandamano yenye mabango
mbalimbali yenye jumbe za kuhamaisha ushirikishwaji wa wanawake kwenye
sekta muhimu nchini yakihudhuriwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu.
Akizungumzia
siku ya wanawake duniani, Afisa Mwandamizi wa Shirika la Posta Aneth
Mdimu amesema Shirika la Posta litaendelea kuwa na usawa kwa wote katika
kutoa ajira kwa wanawake.
Amesema,
katika taasisi yao usawa kwa wote imekuwa ni sera yao kubwa sana na
wamekuwa na wanawake wengi sana katika vitengo mbalimbali wakifanya kazi
zao kwa ustadi mkuu.
"
Ukiangalia katika taasisi yetu kuna Mkurugenzi wa Kibiashara ambaye ni
mwanamke bodi ya wakurugenzi iliona kuna haja ya kuwa mwanamke kwani
wanaweza kwa hilo tunawashukuru sana,"
Mdimu
amesema, ukiangalia katika ngazi ya mikoa kuna wanawake wengi
wanaosimamia taasisi yao hilo limetokana na Uongozi wa Shirika la Posta
kuona wanawake wanatosha katika kuliendesha gurudumu la maendeleo.
"
Asilimia kubwa ya pato la taasisi tunaingiza sisi wanawake, tupo katika
kila kitengo na ukimkuta mwanamke akifanya kazi zake bila wasiwasi wala
kuhitaji msaada kutoka kwa mtu yoyote, tunajivunia," amesema
Aidha,amesema
kuwa wanawake katika shirika la Posta wamejizatiti kufanya kazi kwa
uweledi mkubwa bila kuwezeshwa, wamejipanga kuhakikisha wanafikisha
asilimia 98 ya wanawake katika taasisi hiyo.
Mdimu
ameongezea, wanaishukuru taasisi kwa kuwajali na kuwalinda wanawake
hata kipindi cha afya ya uzazi imekuwa inamtunza Mwanamama kwa kupata
stahiki zake zote na hata akirejea kazini amekuwa anapata muda wa
kunyonyesha.
Machi 08,
kila mwaka dunia nzima imekuw inaadhimisha siku ya wanawake dunian
wakija na kauli mbiu mbalimbali zikihamasisha wanawake wapatiwe usawa
katika sekta mbalimbali ambapo kwa mwaka huu imejikita katika "wanawake
na uongozi chachu ya kufikia dunia yenye usawa"
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...