Katika kuadhimisha kusherehekea siku ya Wanawake Duniani 2021, wasanii mbalimbali wa muziki wa kizazi kipya hapa nchini wamekipongeza kinywaji cha Konyagi kwa kuwapa fursa ya kuthamini ujasiri, ushupavu na uthubutu wa wanawake ambao wamejitoa katika mafanikio ya kazi zao za kimuziki na kuwajenga katika Maisha kiujumla.

Mmoja wa wasanii hao, John Simon Mseke, au maarufu kama Joh Makini, ‘Mwamba wa Kaskazini’, ameishukuru Konyagi kwa fursa iliyompa ya kumzungumzia mwanamke ambaye anaamini amekuwa na mchango mkubwa katika maisha yake na amesema mama yake mzazi ndio kila kitu kwake na anabaki kuwa mwanamke wa nguvu katika maisha yake.

Joh Makini, mzaliwa wa jijini Arusha, ambaye anajulikana kwa wimbo kama "Popote Chochote" anasema mama yake amekuwa ndio kioo chake tangu akiwa mtoto mpaka sasa akiwa mwanamuziki maarufu.

‘Siwezi kumaliza maneno nikiamua kumzungumzia mama huyu shupavu,” Amesema Joh. “Mimi mwenyewe ni mzazi pia, hivyo najua changamoto alizopitia mama yangu wakati nikiwa tumboni, aliponizaa na wakati akinilea.” anasema mkali huyo ambaye pia ni mwanachama hai wa kundi la "Weusi" kutoka Arusha.

Naye Juma Jux, maarufu kama ‘African Boy’ ambaye ni miongoni mwa wasanii wanaosemekana kulipwa hela nyingi katika show zake,amesema mama yake amekuwa na mchango mkubwa katika safari yake ya kimuziki iliyokuwa na vikwazo vingi vya kukatisha tamaa.

Jux, anayeshirikiana na wanamuziki mbalimbali katika nyimbo zake akiwemo Diamond Platnumz aliyeshirikiana naye katika wimbo unaoitwa ‘Sugua” na ule wa ‘Juu’ alioshirikiana na mpenzi wake wa zamani, Vanessa Mdee, anasema kuna watu wake kadhaa wa karibu, wakiwemo wa familia yake waliomkatisha tama wakati anaanza muziki, lakini mama yake alimwambia anaweza.

“Mama alinifundisha maisha, namna ya kuwajali wanawake wengine na watu wote wanaonizunguka. Licha ya kuwa peke yake, alinipa malezi bora na kunilea,” anaongeza Jux.

“Kwangu mimi, mama yangu ni jasiri ‘ hero’ na kupitia siku hii muhimu, nawatakia wanawake wote heri ya kusherehekea sikukuu ya wanawake Duniani” alimalizia kusema Jux huku akishukuru Konyagi kwa kumpa fursa ya kutambua mchango wa mwanamke huyo muhimu kwake maishani.

Siku ya Wanawake Duniani imegusa kila mtu duniani kutokana na mchango wa akina mama, sio tu katika malezi na kujenga familia bora, bali pia kushiriki shughuli za kiuchumi katika nyenzo na nyanza mbalimbali, ikiwemo kufanya shughuli ambazo zimekuwa zikifanywa na wanaume kama vile udereva, ufundi na nyinginezo nyingi. Konyagi pia imetoa chupa yenye nembo maalumu ya mwanamke aliyeinua mikono kama kiashiria cha kutambua umuhimu wa mwanamke katika jamii.

Katika wasanii wengine waliopata fursa ya kutambua Wanawake muhimu katika Maisha yao ni Msanii Mwasiti ambaye amemtambua Angelique Kidjo kama mwanamke aliyempa ujasiri kwa kazi zake za muziki na mchango katika jamii.

Msanii Snura Mushi pia ametambua watu watatu ambao ni bibi yake, muigizaji Monalisa pamoja na muimbaji wa muziki wa taarab Sabaha Salum.

Mtangazaji wa Clouds FM Mamy Baby pia alimaliza kwa kumtambua DJ Fetty aliyekua akifanya kazi katika kituo hicho kama mwanamke jasiri aliyempa confidence katika tansia ambayo inaongozwa Zaidi na wanaume.

“DJ Fetty ni mfano wa wanawake wengine, akiwa mpambanaji kimaisha  na mwenye mafanikio katika kazi yake iliyopelekea atengeze jina kupitia vipindi mbalimbali kama vile ‘Jahazi’ na vinginevyo vingi.” anasema mtangazaji huyo.

Maelezo ya wasanii hawa yamepewa nguvu na kampuni ya Tanzania Distilleries Limited , inayotengeneza kinywaji cha Konyagi katika kutambua ujasiri, weledi, ushupavu na uthubutu wa mwanamke katika kujiletea maendeleo kupitia shughuli anazofanya katika jamiii inayomzunguka.

Meneja Chapa wa Konyagi inayotengenezwa na kampuni ya Tanzania Distilleries Limited, Pamela Kikuli amesema kinywaji hicho ni kile kile kwa ladha na ubora lakini ameona kuna umuhimu wa kutambua umuhimu wa Wanawake kwa kuweka nembo maalum kwa kipindi hiki maalum.

Siku ya Wanawake Duniani huadhimishwa tarehe 8 Machi ya kila mwaka. Siku hiyo ilianza kuadhimishwa tarehe 8 Machi 1975 baada ya Umoja wa Mataifa kuridhia siku hii kutumika kama siku rasmi ya kuikumbusha dunia juu ya haki za wanawake.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...