Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Mary Masanja akionesha kitabu alichokizindua  katika  warsha ya Utalii endelevu kanda ya Ziwa yenye lengo la kupanua wigo wa Utalii kanda ya Ziwa  ambayo imeandaliwa na Chuo Kikuu cha Dar es salaam, leo Jijini Mwanza.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Mwanza pamoja na wadau wa Warsha ya kupanua wigo wa Utalii Kanda ya Ziwa iliyoandaliwa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ilyofanyika leo Jijini Mwanza.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Mary Masanja   akikata utepe kuzindua Kitabu cha ‘Utalii Endelevu Tanzania’ kilichoandikwa na Wanufaika wa Mradi Utalii wa SIDA wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wakishirikiana na Watafiti wa Gothernberg kutoka nchini Sweeden   wakati wa  Uzinduzi wa  Warsha ya Utalii Endelevu Kanda ya Ziwa ambayo imeandaliwa na Chuo hicho Jijini Mwanza.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja akizungumza kuhusu Warsha ya Kupanua Wigo wa Utalii Kanda  Ziwa Iliyoandaliwa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambapo amesema Warsha hiyo itakua na faida kwa mikoa yote sita ya Kanda ya Ziwa katika kuongeza Idadi ya Watalii na kuinua sekta ya Utalii nchini.
 
*************************************

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja amewataka watafiti kutoka Chuo Kikuu cha Dar-es-Salaam(UDSM) waongeze nguvu katika  kufanya tafiti zitakazoibua na kugundua vivutio vipya vya Utalii katika mikoa ya Kanda ya ziwa. Mhe. Masanja ameyasema  hayo wakati wa ufunguzi wa Warsha ya Utalii Endelevu Kanda ya ziwa iliyofanyika katika Chuo cha Taifa cha Utalii mkoani Mwanza.

Katika hotuba yake, amewapongeza watafiti wa ndani walioamua kujikita kufanya tafiti katika Kanda hiyo zinazoisaidia Sekta ya Utalii akibainisha kuwa jukumu hilo ni muhimu katika ulimwengu wa sasa ambao una ushindani mkubwa katika soko la Utalii. ‘’Watafiti mnatakiwa kufanya tafiti zitakazosaidia kuainisha bidhaa za utalii katika mikoa yote sita ya Kanda ya Ziwa” Amesema Mhe. Masanja.    

Amesema, Serikali inatarajia kuendeleza na kuvitangaza vivutio vyote vya  Utalii vilivyoko Kanda ya Ziwa.   Aidha, amebainisha kuwa imeyapandisha hadhi baadhi ya maeneo  yaliyokuwa Mapori ya Akiba yawe Hifadhi za Taifa hatua  iliyoongeza idadi ya Hifadhi za Taifa hadi kufikia  22 mwaka 2020 toka 16 zilizokuwepo mwaka 2015.

Amesema katika eneo la Kanda ya Ziwa Serikali imefanikiwa kuanzisha Hifadhi za Taifa mpya sita ambazo ni Burigi-Chato, Ibanda Kyerwa, Mto Ugala, Kigosi Moyowosi, Nyerere na Rumanyika-Karagwe na kuimarisha mtandao wa Utalii katika Kanda ya Ziwa ambapo sasa kuna  jumla ya Hifadhi za Taifa nane (8) ikiwemo Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Rubondo, Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Saanane, Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.

 Amesema ili kufanikisha shughuli za Utalii hapa nchini, Serikali kupitia taasisi zake itaendelea kuwashirikisha na kuwatumia kikamilifu watafiti na Sekta Binafsi”.  Ameupongeza Uongozi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa kufanikisha Jukwaa la kuendeleza Utalii Kanda ya Ziwa.
 
Kwa upande wake Mkurugenzi  Mtendaji wa Makumbusho ya Taifa, Dk Noel Lwoga amesema Kanda ya Ziwa ina vivutio vingi sana lakini bado havijaendelezwa. Amesema Kanda ya Ziwa ina ina utajiri mkubwa wa vivutio vya Utalii mbali na Misitu na Wanyamapori.

Mratibu wa mradi wa SIDA kutoka  Chuo Kikuu cha Dar-es-salaam(UDSM), Prof. Wineaster Anderson amesema kupitia mradi wa Utafiti katika Utalii Endelevu wanafanya tafiti za kuibua bidhaa za Utalii katika mikoa ya Simiyu,Mara na Shinyanga. Amesema kupitia mradi huo, wameweza kufadhili wahitimu nane katika masomo ya PHD.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...