Baadhi ya wazee wakimsikiliza mbunge wao alipokutana nao ili kupata maoni na mapendekezo atakayokwenda nayo bungeni.

Na Amiri Kilagalila,Njombe
WAZEE wilayani Ludewa wameilalamikia serikali kwa kuwahamasisha kukata bima ya afya CHF iliyoboreshwa lakini wamekuwa wakishindwa kupata dawa kutokana na uhaba wa madawa kwenye maeneo ya kutoa huduma za afya huku wakilazimika kununua kwenye maduka binafsi licha ya kuwa na bina hiyo iliyoghalamiwa shilingi 30,000.

Wazee wametoa changamoto hiyo ya kushindwa kupata huduma ya madawa licha ya kuwa na bima ya afya katika mkutano na mbunge wao Joseph Kmaonga alipokutana nao ili kupokea changamoto zao na mapendekezo ili kuziwasilisha katika bunge la bajeti linalotarajiwa kuanza karibuni.

Witijadi Luwili na Stiven Kalinjila ni baadhi ya wazee wastaafu wamesema licha ya serikali kuwa na mpango mzuri wa kutoa huduma pamoja na kuboresha miundombinu ya afya lakini changamoto kubwa kwao imekuwa ni upatikanaji wa madawa unaowalazimu kununua madukani licha ya kuwa na bima ya afya.

“Tatizo ninaloliona katika hospitali zetu ni moja majengo yako safi,wahudumu wako safi lakini kinachoshindikana ni madawa hakuna,unafika pale wakati mwingine unafika na bima yako kufika kwenye dirisha unaambiwa uende ukanunue dawa hapa haipo,ninaomba huduma iboreshwe ili wateja wapate kuridhika”alisema Witijadi Luwili

Naye Stiven Kalinjila amesema “Tunaomba huko vitoa hivyo vifanye kazi na vijitosheleze kwa vifaa tiba na wataalamu,vituo tumejenga lakini kama vifaa tiba hakuna inakuwaje,tuombe hilo lifuatiliwe ili tiba ipatikane”

Vile vile wengine wamesema wamekuwa wakikabiliwa na changamoto ya kukosa huduma licha ya kuwa na bima hiyo wanapokwenda katika hospitali za kawaida huku wengine wakiiomba serikali kutoa elimu zaidi juu ya ufanyaji kazi na mipaka ya bima.

Licha ya changamoto hiyo lakini mwenyekiti wa wazee wilayani humo Onesmo Haule kwa niaba ya wazee wengine ameiomba serikali kusaidia kuboresha sekta ya uvuvi katika ziwa nyasa ikiwa sambamba na kuwaboreshea wavuvi zana uvuvi pamoja na kufungua mipaka ya kibiashara baina ya Tanzania na nchi ya Malawi kupitia ziwa Nyasa ili kusaidia kukuza uchumi wa wilaya ya Ludewa na Tanzania.

Kwa upande wake mbunge wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga,amesema ataendelea kufuatilia changamoto hiyo kwa kuwa wananchi wengi wameendelea kulalamika kwa kukosa dawa licha ya kuwa na bima huku wengine wakata tamaa ya kuwa na bima ya afya.

“Hiki kitu kinawakera sana wananchi na muda mwingine hawaoni faida ya kuwa na hizi bima,wakati mwingine dawa zipo lakini wananchi wanaambiwa wakanunue dawa kuna viongozi wangu wa Chama siku walitengeneza mgonjwa feki akaandikiwa dawa vizuri lakini kwenda dirisha la dawa anaambiwa dawa hakuna wakati kuna siku tatu tu nimetembelea na kukukuta dawa kwa hiyo kuna shida tunaendelea kufuatilia”alisema Kamonga.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...