Na Amiri Kilagalila,Njombe

Wazee na wachungaji wa madhehebu mbali mbali wilayani Ludewa mkoani Njombe wameiomba serikali kupitia wizara ya mambo ya ndani kukamilisha ujenzi wa nyumba za polisi zilizoanza kujengwa mwaka 2007 na kusimama kutokana na sababu mbali mbali huku zikiendelea kuharibika.

Padree Ditraum Mwinuka kutoka kanisa katoliki jimbo la Njombe kupitia uwakilishi wa udekano wa Lupingu ni miongoni mwa watumishi walioomba serikali kupitia kikao na mbunge wao Joseph kamonga kilichofanyika mjini hapo kukamilisha nyumba hizo huku wakidai zimekuwa zikiharibu taswira ya mji wakati kodi za wananchi zimepote kwa ajili ya ujenzi  wa Nyumba hizo.

Aidha wamesema askari polisi wamekuwa wakipata shida kuishi katika nyumba za kupanga wakati serikali imekuwa na dhamira njema ya kuwaweka karibu na mazingira ya kazi kwa kuwaboreshea makazi lakini kushindwa kukamilika kwa majengo hayo kwa miaka mingi kunaleta sintofahamu kwa wakazi wa Ludewa mjini.

Kwa upande wake mbunge wa Jimbo la Ludewa wakili Joseph Kamonga ameahidi kushughulikia swala hilo la ukamilishaji wa nyumba hizo za Polisi ili kuongeza ufanisi kwa jeshi kwa kuishi karibu pamoja na kuboreshewa makazi.

“Nilishapata nafasi ya kukaa na naibu waziri wa mambo ya ndani na hata mkuu wa kituo hapa Ludewa aliongea nae kuelezea changamoto ya hizi nyumba zimetelekezwa kwa muda mrefu na zinapunguza sana ufanisi wa kazi wa jeshi letu”alisema Kamoga

Aliongeza kuwa “Ni vema askari wasizoeene sana na rai kwa kukaa karibu,na wakikaa hapa hata kutekeleza majukumu yao itakuwa ni rahisi hivyo ninaamini wataweza kuzimalizia”alisema Kamonga


Baadhi ya majengo ya nyumba za jeshi la polisi wilayani Ludewa zilizoanza kujengwa mwaka 2007 na kutelekezwa,mbunge wa Ludewa ameahidi kushughulikia swala la ukamilishaji wa Nyumba hizi.

Mbunge wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga akifafanua kuhusu ukamilishwaji wa nyumba za polisi na faida zake katika kuimarisha ufanisi wa kazi wa jeshi ndani ya wilaya ya Ludewa


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...