Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama akiwasikiliza  wafanyakazi wa wa kiwanda cha kuzalisha chumvi cha Neelkanth Salt Limited, mkoani Pwani, wakati walipotembelea kiwanda hicho kujionea hali ya urutubishaji wa chumvi na amemwagiza Afisa kazi na timu yake kufika kiwandani hapo kutatua changamoto za kutokuwa na vyama vya wafanyakazi, vitendea kazi na mikataba ya ajira pamoja na michango kutopelekwa NSSF.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama akiongea na wafanyakazi wa wa kiwanda cha kuzalisha chumvi cha Neelkanth Salt Limited, mkoani Pwani, wakati walipotembelea kiwanda hicho kujionea hali ya urutubishaji wa chumvi na kuwataka wamueleze changamoto zinazowakabili kwenye ajira yao.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama akiwa anaongea na  Afisa Kazi  na Meneja wa NSSF mkoa wa Dar es salaam huku akiwapa maelekezo pamoja na Afisa Rasilimali watu wa Kampuni ya Unique Consultants Services, Isaya Vangisheria kutatua kutatua changamoto za  wafanyakazi wa Kampuni ya Unique Consultants Services wakati walipomsimamisha kueleza changamoto zao za ajira, jijini Dar es salaam.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama akimpigia simu Afisa Kazi na Meneja wa NSSF mkoa wa Dar es salaam na amewapa maelekezo ya kutatua kutatua changamoto za  wafanyakazi wa Kampuni ya Unique Consultants Services wakati walipomsimamisha kueleza changamoto zao za ajira, jijini Dar es salaam.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama akisoma malalamiko ya wafanyakazi wa Kampuni ya Unique Consultants Services walipo usimamisha msafara wake ili kueleza changamoto zao mahaha la pa kazi,  jijini Dar es salaam.

*****************************************

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama amekerwa na waajiri nchini wasiotekeleza Sheria na.6 ya mwaka 2014 kama ilivyofanyiwa marejeo mwaka 2019, sheria hiyo inamtaka mwaajiri kumpa mkataba wa ajira mfanyakazi pamoja na kutoa haki ya kuwa na vyama vya wafanyakazi.

Waziri Mhagama akiwa katika ziara ya kujionea hali ya urutubishaji vyakula kwenye viwanda vikubwa vya usindikaji wa chakula (Unga wa ngano, unga wa mahindi na mafuta ya kula) jijini Dar es salaam, wafanyakazi wa kiwanda cha kuzalisha chumvi cha Neelkanth Salt Limited pamoja na Kampuni ya Unique Consultants Services, wamejitokeza kueleza kero zao zilizojikita kwenye mikataba ya ajira, kutokuwepo na haki ya vyama vya wafanyakazi, kima cha mshahara pamoja na michango yao kutopelekwa NSSF.

“Afisa kazi mkoa wa Pwani  nakupigia hii simu nikiwa hapa kwenye kiwanda cha Neelkanth Salt Ltd nataka kesho uje hapa na timu yako nataka mkague mikataba, hakikisheni kinaundwa chama cha wafanyakazi, angalia mishahara  na posho zinazingatia kazi wanazofanya, angalieni vitendea kazi. Huyu mwekezaji anafanya kazi nzuri hapa nchini na amewekeza hadi Tanga, lakini tunataka uwekezaji wenye tija uendane na kazi zenye staha kwa watanzania” Amesisitiza Mhe. Mhagama.

Baada ya kuongea na wafanyakazi wa Kampuni ya Unique Consultants Services, Waziri Mhagama alipiga simu hapo hapo na kumwelekeza Afisa kazi wa mkoa wa Dar es salaam ndani ya saa moja kuhakikisha anafanya ukaguzi wa ghafla kuwasikilza wafanyakazi hao kero zao.

“Watanzania wanao wajibu wa kutafuta haki zao mahala pa kazi, nataka Afisa kazi Dar e salaam uje hapa na meneja wa Tawi wa NSSF, kwani nimeelezwa wafanyakazi hawa kwa miaka miwili michango yao ya mishahara haipelekwi NSSF.Pia nipewe taarifa ya utekelzaji wa suala hili mara moja likikamilika. Niwatake wafanyakazi mtulie serikali inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli ipo tayari kushughulikia kero za wananchi kwa wakati” Amesema Mhagama.

Katika hatua nyingine, Waziri Mhagama amewataka waajiri kuhakikisha michango ya mishaha ra ya wafanyakazi inapelekwa kwenye Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) kwa mujibu wa sheria. Sheria ya Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya jamii sura na. 50 kama ilivyofanyiwa marejeo mwaka 2018, inakata mwajiri awasilishe michango ya wafanyakazi kwenye mfuko huo kila mwenzi ambapo mwajiri  na mwajiriwa kila mmoja huchangia 10% ya mshahara.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...