Waziri wa Kilimo Prof. Adolf Mkenda akiongea watumishi na wafanyakazi wa kiwanda cha sukari cha Manyara ambapo amekipongeza kwa kuweza kuzalisha tani 8,133 mwaka 2021 toka tani2,700 mwaka 2015/16  za sukari huku kikinunua miwa yote ya wakulima .Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Babati Lazaro Twange na Mwenyekiti wa Bodi ya Sukari Bi.Mwamini Juma
Waziri wa Kilimo Prof. Adolf Mkenda akizungumza na menejimenti ya kiwanda cha sukari TPC cha Moshi jana ambapo amekipongeza kwa kuwekeza katika miundombinu ya kisasa ya umwagiliaji na matumizi ya mbegu bora hali iyosaidia kuongeza tija na uzalishaji sukari toka tani 88,968,000 mwaka 2019/20 hadi tani 101,403 mwaka 2021 huku ikilipa gawio serikalini la shilingi Bilioni 15 mwaka 2021 tofauti na viwanda vingine vikubwa vya sukari.
Mkuu wa Wilaya ya Babati Mhe. Lazaro Twange akitoa taarifa ya sekta ya kilimo kwa Waziri wa Kilimo Prof. Adolf Mkenda (kushoto) jana ambapo amesema kilimo na madini ndizo shughuli zinazoajili wananchi wengi wa  Babati hivyo ameomba serikali kuongeza kasi ya kuvutia wawekezaji kujenga viwanda vidogo vya sukari ili kuwa na uhakika wa soko la miwa ya wakulima.
Afisa Mtendaji Utawala kiwanda cha sukari TPC Moshi Bw. Jafar Ali akizungumza na waandishi wa habari jana wakati wa zara ya Waziri wa Kilimo kiwandani hapo. Bw. Jafar alisema kiwanda hicho hadi kufika Huni 2020 kimewekeza Bilioni 226 kuboresha na kupanua uwezo wa kiwanda hali iliyokuza uzalishaji wa sukari.
Waziri wa Kilimo Prof. Adolf Mkenda akizuru kukagua kiwanda cha sukari cha Manyara kilichopo Wilaya ya Babati jana ambapo amekipongeza kwa kuwekeza katika kilimo cha umwagiliaji na kusaidia wakulima wadogo kupata soko la uhakika la miwa.
Baadhi ya wakulima wadogo wa miwa wa kijiji cha Matufa kwenye bonde la Babati wakiwa kwenye mkutano wa Waziri wa Kilimo Prof. Adolf Mkenda jana alipowatembelea ambapo ameahidi kuwa serikali inatafuta wawekezaji wa viwanda vya sukari vingi ili kuinua soko la miwa yao. (Picha na Wizara ya Kilimo)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...