Mkuu wa Wilaya ya Kasulu Kanali Simon Anange pamoja na Katibu tawala wa wilaya ya Kasulu, Joseph Kashushura, Tarehe 3 Machi, 2021 wamepokea ujumbe kutoka wizara ya Viwanda na Biashara, EPZA, TIC na Bodi ya Sukari ulioambatana na mwakilishi mkazi wa kampuni ya Mahashree Agroprocessing Tz Ltd mwenye nia ya kuwekeza kiwanda cha sukari na kilimo cha miwa.

Ziara hii imekuja mara baada ya agizo la Rais Dk John Magufuli aliyoitoa tarehe 12 Februari, 2021 alipokuwa akizindua kiwanda cha nafaka cha Mahashree Agroprocessing Tz Ltd kilichopo Mkoani Morogoro.

Rais aliiagiza Wizara ya viwanda na Biashara kwa kushirikiana na EPZ na TIC kuhakikisha wanampatia mwekezaji ambaye ni Mahashree Agroprocessing Tz Ltd eneo zuri kwa ajili ya kilimo cha miwa na ujenzi wa kiwanda cha sukari ili kuongeza uzalishaji wa sukari nchini, kuleta ajira na kodi kwa serikali.

Katika kutekeleza agizo hilo la Rais, Wizara ya Viwanda na Biashara kwa kushirikiana na Kituo cha Uwekazaji (TIC) ilifanya jitihada za upatikanaji wa shamba ambalo linapakana na mto Malagalasi lenye ukubwa wa hekta 37,662. Shamba hili lipo katika kata tatu za Heru Ushingo, Kitanga na Nyamidaho zenye vijiji saba ambavyo ni Nyarugusu, Kiyungwe, Kitanga, Kumtundu, Nyamidaho, Kigadye na Heru Ushingo.

Baada ya kuzungunguka na Mkurugenzi Mkazi wa kampuni ya Mahashree ndugu Dhaval Maheshwari katika eneo la mradi ambalo lipo umbali wa kilometa 70 hadi 110 kutoka Makao makuu ya Wilaya ya Kasulu.

Mwakilishi huyo wa mwekezaji amevutiwa zaidi na shamba hili ambapo amesema kuwa kwa sasa watafanya upembuzi yakinifu ya ardhi na wakishakamilisha wataanza na kilimo cha miwa na ujenzi wa kiwanda cha sukari ambapo kwa kiasi kikubwa watahusisha wanakijiji wanaozunguka eneo la mradi kushiriki pia katika kilimo cha miwa (Out Growers) kwa ajili ya malighafi ya kiwanda.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilzaya ya Kasulu, Kanali Simon Anange amepogeza jitihada zinazofanywa na Wizara ya Viwanda na Biashara, TIC, EPZA na Bodi ya Sukari (SBT) kwa kulichagua eneo la Kasulu kuwa kitovu cha uwekezaji kwa kumleta mwekezaji ambaye ameonesha nia ya kuwekeza katika kilimo cha miwa na ujenzi wa kiwanda cha sukari.

Naye Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara, Prof Riziki Shemdoe amefanya mazungumzo na mwakilishi wa mwekezaji na kumhakikishia ushirikiano wa kila hatua ili kuhakikisha uwekezaji huu mkubwa unaanza mapema kwani Kigoma ni eneo zuri la uwekezaji hasa ukizingatia uwepo wa mto malagalasi ambao unatiririsha maji ya kutosha na uwepo wa reli kwa ajili ya usafirishaji wa mashine za kiwanda na bidhaa.




*

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...