Na Amiri Kilagalila,Njombe

Wakulima kote nchini wamehamasishwa kuchangamkia fursa ya kilimo cha zao la vanilla ambalo uhitaji wake duniani ni mkubwa zaidi licha ya kwamba upatikanaji wa wa zao hilo kwa sasa umekuwa ni adimu.

Vanilla, Si zao ambalo limezoeleka haswa katika maeneo mengi nchini  licha ya kwamba si geni masikioni mwa wengi.    Ni zao ambalo uazalishaji wake umekuwa ni kidogo sana nchini pengine hata katika mataifa mengine kiasi kwamba gharama yake kwa sasa imepanda maradufu hadi kufikia shilingi mil.1 kwa kilo moja ya vanilla.

Kufuatia hali hiyo  Magreth Mgina meneja mahusiano wa kampuni ya Vanila International amechukua jukumu la kuhamasisha wakulima kuchangamkia fursa hiyo huku baadhi ya wakulima mkoani Njombe wakianza kuchangamka na fursa

“Tunawahamasisha sana wakulima hasa vijana kila mtu anayependa kujifunza na tunatoa elimu bure kuhusu kilimo hiki”

Zao la vanilla lina umuhimu haswa katika utengenezaji wa yoghati, keki vinywaji aina ya wine na vilevile maandazi.

Msanii uigizaji sauti maarufu ka jina la Baraka magufuli amepata nafasi ya kuzungumza na wakazi wa Njombe huku msisitizo akiuweka katika uzalishaji wa Vanilla.

“Niendelee kuhamasisha watanzania wote kwasababu mimi nimejionea hapa Njombe jinsi zao linavyplimwa,niombe tuhakikishe tunalima kwasababu zao hili pia lina thamani kubwa kwa sasa”alisema Baraka Magufuli

Uthubutu katika jitihada za kutafuta mafanikio ni hatua mojawapo katika kuyasogelea mafanikio, ambapo Gloria Haule huyu ni mama ambae amethubutu kujikita katika zao la vanilla, ameeleza matarajio yake katika kilimo hicho

“Kwa kweli mimi nilihamasishwa baada ya kusikia matangangazo hata kanisani,kwa hiyo matarajio yangu hapo baadaye niweze kufika mahali Fulani ambayo ni nzuri zaidi kuliko sasa”

Licha ya kuhamasisha wakulima kote nchini kuchangamkia fursa hiyo kampuni ya vanilla international inayopataikana katika maeneo ya kanisa la Anglican mjini Njombe,inatoa elimu bure kwa wale watao kuwa tayari kujikita katika zao hilo huku wakiwahakikishia upatikanaji wa soko kwa asilimia 99.9.

“Zao la Vanilla ni zao la fedha nyingi na kilo moja imeweza kufika mpaka zaidi ya milioni moja niwaombe sana wakulima kuwasiliana na sisi ili tuweze kuwasaidia katika kilimo”alisema Simon Mukondya mkurugenzi wa Vanilla International Ltd

Vanilla huchukua muda wa miezi mitatu tu tangu kupandwa hadi mavuno na gharama yake kila kilo moja inatajwa kufikia sh.laki 9 hadi mil.1 kwa sasa.

Zao la Vanilla lililoanza kulimwa kwa sasa mkoani Njombe kutokana na kuendelea kuhamasishwa ili kulima kilimo hicho kutoka na thamani yake.

Mmea wa zao la Vanilla kama ulivyopigwa na mpiga picha wetu mjini Njombe mara baada ya zoezi la uhamasishaji lililofanywa na kampuni ya Vanilla International Ltd


Simon Mukondya mkurugenzi wa Vanilla International Ltd wakati akifafanua faida na matumizi ya zao hilo huku akiwaomba wakulima wanaopenda kujihusisha na kilimo hicho kuweza kuwasiliana kwa kuwa kampuni hiyo imekuwa ikifanya shughuli zote za kilimo na kumkabidhi mkulima shamba likiwa tayari kwa kuendelea kulitunza.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...