Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV

KOCHA Nasreddine Nabi raia wa Tunisia 🇹🇳 rasmi ametua nchini leo April 20, 2021 siku ya Jumanne tayari kukinoa Kikosi cha Wananchi, Young Africans katika mashindano mbalimbali msimu huu ambayo timu hiyo inashiriki.

Kocha huyo ametua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, Dar es Salaam majira ya Saa 9 Alasiri, na kupokewa na moja ya Kiongozi wa timu hiyo kutoka katika Kampuni ya GSM, Eng. Hersi Said.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Uwanjani hapo, Terminal III, Kocha Nasreddine Nabi amesema amekuja nchini kuinoa Yanga SC baada ya kuwepo na makubaliano kati yake na Viongozi wa Klabu hiyo, Nabi amesema amefurahi kufika nchini Tanzania kuja kuifundisha timu hiyo ya Wananchi sambamba na mapokezi aliyoyapata katika uwanja wa Ndege.

Amesema anajivunia kuja kuinoa Klabu kubwa barani Afrika yenye idadi kubwa ya Wachezaji wanaotambulika Afrika na yenye idadi kubwa ya Mashabiki hapa nchini. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...